MSHAMBULIAJI wa Liverpool, Mario Balotelli alitolewa nje katika mchezo wa kirafiki ambao mashabiki hawakuhudhuria dhidi ya Wolves baada ya kuanza kuzozana na refa Chris Foy.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, aliyehamia Anfield kutoka AC Milan kwa Pauni Milioni 16 mwezi uliopita, alizuiwa na Kolo Toure wakati Foy akizungumza naye kwenye mchezo huo Melwood.
Chanzo cha mzozo huo ni baada ya Mtaliano huyo kugongana na mchezaji wa Wolves. Baada ya mzozo huo tu, Balotelli alitolewa nje mara moja.
Balotelli akielekea nje baada ya mzozo huo
Toure aliweka bega lake kumdhibiti mchezaji mwenzake huyo wa zamani wa Manchester City asiendelee kuzozana na Foy juu ya tukio hilo kabla ya Balotelli kutolewa aingie mchezaji mwingine.
Nyota huyo wa zamani wa Inter Milan alianza pamoja na wachezaji kama Adam Lallana, Jose Enrique na Lucas Liverpool ikishinda 1-0 dhidi ya timu ya Daraja la Kwanza, bao pekee la Lallana.
Balotelli alichukua mpira kwenye himaya ya kipa wa Wolves katika mchezo huo
Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester City aliisumbua mno gnome ya Wolves katika mchezo huo
0 comments:
Post a Comment