Rais wa TFF, Leodegar Tenga akinywa maji ya Uhai, wadhamini wa michuano ya vijana ya Ligi Kuu |
Na Prince Akbar
MICHUANO ya
kuwania Kombe la Uhai inayoshirikisha wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 wa
klabu za Ligi Kuu ya Vodacom inaanza kutimua vumbi kesho (Desemba 11 mwaka huu)
kwenye viwanja viwili tofauti.
Viwanja
vitakavyotumika kwenye michuano hiyo ni Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume na
Uwanja wa Azam ulioko Chamazi. Viwanja vyote viko Dar es Salaam.
Timu hizo
zimegawanywa katika makundi matatu ya michuano hiyo itakayomalizika Desemba 23
mwaka huu. Kundi A lina timu za Coastal Union, JKT Ruvu, Mtibwa Sugar, Tanzania
Prisons na Toto Africans.
Kundi B ni
African Lyon, Azam, Mgambo Shooting, Polisi Morogoro na Simba, wakati timu za
Kagera Sugar, Oljoro JKT, Ruvu Shooting na Yanga zinaunda kundi C.
Mechi za
fungua dimba kundi A ni Coastal Union vs Tanzania Prisons (saa 2 asubuhi-
Karume), JKT Ruvu vs Mtibwa Sugar (saa 10 jioni- Karume). Kundi B ni African
Lyon vs Polisi Morogoro (saa 3 asubuhi- Chamazi) na Azam vs Mgambo Shooting
(saa 10 jioni- Chamazi).
Kundi C
litaanza mechi zake Desemba 12 mwaka huu ambapo Kagera Sugar itacheza na Oljoro
JKT saa 8 mchana- Karume wakati Yanga na Ruvu Shooting zitakuwa kwenye Uwanja
wa Chamazi kuanzia saa 10 kamili jioni. (Ratiba nzima imeambatanishwa)