Thursday's gossip column

TRANSFER GOSSIP

BEKI wa Chelsea, David Luiz anawaniwa na vigogo wa Hispania, Barcelona na anaweza kuondoka mwishoni mwa msimu, licha ya kuwa msimu usiovutia sana mwanzoni Stamford Bridge.
KIUNGO wa kimataifa wa Mali na Barcelona, Seydou Keita, mwenye umri wa miaka 32, inafikiriwa anatakiwa na Liverpool, ingawa anaweza kuipiga chini ofa ya Anfield na kutimkia AC Milan.
MCHEZAJI anayegombewa na Manchester City na Chelsea, Ezequiel Lavezzi, mwenye umri wa miaka 27, yuko tayari kuondoka Napoli baada ya kuibuka tetesi za kutofautiana na rais wa klabu hiyo, Aurelio de Laurentiis.
WAKALA wa Nemanja Vidic, Silvano Martina ametupilia mbali uvumi kwamba, nahodha huyo wa Manchester United atahamia Juventus.
Nyota wa Sochaux, Marvin Martin, anatarajiwa kuviba pengo la  Eden Hazard katika klabu ya Lille, ikiwa kiungo huyo atahamia Arsenal ya England mwishoni mwa msimu.
NAHODHA wa Montpellier, Mapou Yanga-Mbiwa ameripotiwa kuendelea nia yake ya kuchezea Manchester United au Arsenal msimu ujao.
KLABU ya Tottenham inaweza kuingia kwenye vita na Benfica na Inter MIlan kuwania saini ya kiungo wa PSV, Georginio Wijnaldum, mwenye umri wa miaka 21, ambaye ni Mholanzi anayewezwa kuuzwa kwa dau la pauni Milioni 20.
KLABU ya Asrenal imeungana na orodha ndefu ya klabu zinazotaka mshambuliaji wa SC Heerenveen, Bas Dost, ambaye amekataa ofa ya Aston Villa akitaka kujiunga na klabu kubwa.

OTHER GOSSIP

KIUNGO wa Rennes, Yann M'Vila alilazimika kukosa mechi ya timu yake na Ajaccio mwishoni mwa wiki baada ya kukamatwa na Polisi akituhumiwa kumpiga kijana mdogo.
Kocha wa England, Roy Hodgson anatumai kubadilisha uamuzi wa kipa wa West Brom, Ben Foster kustaafu soka ya kimataifa na kurudi kuitimikia Three Lions, ingawa mzuia michomo huyo wa The Baggies anaonekana kama hatabadili msimamo wake.
MCHEZAJI mpya wa Arsenal, Lukas Podolski amesema kwamba alikataa ofa kibao kutoka klabu kubwa Ulaya, ili atue Emirates na kuungana na Mjerumani mwenzake, Per Mertesacker wanayecheza naye hadi timu ya taifa.

AND FINALLY

MCHEZAJI namba moja wa tenisi Uingereza, Andy Murray na beki wa zamani wa Manchester United, Gary Neville ni miongoni mwa waliolikandia gazeti la The Sun kuweka ukurasa wa mbele habari ya kuteuliwa kwa Hodgson kuwa kocha wa England.