• HABARI MPYA

    Sunday, May 20, 2012

    FERGUSON AKIMBIZWA HOSPITALI AKIVUJA DAMU


    Sir Alex Ferguson
    Sir Alex Ferguson
    Published: Today at 01:41

    KOCHA wa Manchester United, Sir Alex Ferguson alikimbizwa hospitali jana usiku.

    Alikuwa kwenye kwenye tamasha la soka wakati anakimbizwa hospitali baada ya kuanza kutokwa damu nyingi puani bila kukoma.
    Fergie — aliyefanyiwa tiba ya matatizo ya moyo mwaka 2003 — alichukuliwa na ambulance kukimbizwa hospitali mjini Glasgow, Scotland nyumbani alipo kwa mapumziko hivi sasa.
    Tukio hilo lilitokea akiwa anazungumza katika hoteli ya Thistle Hotel katika hafla ya chakula cha usiku kusherehekea miaka 40 tangu klabu ya Rangers itawe Kombe la Washindi Ulaya.
    Kiasi cha wageni 1,000 waliambiwa dakika za mwishoni kwamba ameondoka kutokana na matatizo binafsi.
    Fergie, ambaye aliichezea Glasgow miaka ya 1960, alionekana akitokwa damu akiwa na mchezaji mwenzake wa zamani wa Rangers, Sandy Jardine na kocha wa zamani Alex McLeish.
    Fergie alitibiwa kwa muda na kuruhusiwa na madaktari wakasema hayakuwa matatizo makubwa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: FERGUSON AKIMBIZWA HOSPITALI AKIVUJA DAMU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top