TIMU ya Argentina imeendeleza wimbi la ushindi katika Fainali za Kombe la Dunia baada ya kuichapa Austria mabao 2-0 katika mchezo wa Kundi J usiku huu Uwanja wa AT&T, Arlington, Texas, Marekani.
Ilikuwa siku nyingine nzuri kwa mshambuliaji wa Inter Miami ya Marekani, Lionel Andrés Messi ambaye keshokutwa anatimiza umri wa miaka 39 aliyefunga mabao yote mawili dakika ya 38 na 90’+5, ingawa pia alikosa penalti dakika ya tisa.
Messi sasa amefikisha mabao 18 aliyofunga kwenye Fainali za Kombe la Dunia na sasa anaongoza kwenye historia ya wafungaji Bora wa muda wote, akimpita gwiji wa Ujerumani, Miroslav Klose anayebaki na mabao yake 16.
Kwa ushindi huo, Argentina inafikisha pointi sita na kuendelea kuongoza Kundi J ikifuatiwa na Austria yenye pointi tatu na Jordan na Algeria zitakazomenyana kesho Asubuhi Uwanja wa Levi's, Santa Clara, California, Marekani, ambazo zote hazina pointi baada ya kupoteza mechi zao za kwanza.



.png)
0 comments:
Post a Comment