• HABARI MPYA

    Monday, June 22, 2026

    MAFARAO WA MISRI WAKIWASHA KOMBE LA DUNIA, WAICHAPA NEW ZEALAND 3-1


    TIMU ya Misri imeichapa New Zealand mabao 3-1 katika mchezo wa Kundi G Fainali za Kombe la Dunia Asubuhi ya leo Uwanja wa BC Place, Vancouver nchini Canada. 
    New Zealand waliuanza vyema na kwa bahati mchezo huo wakianza kupata bao lililofungwa na beki wao tegeo wa kati, Finn Surman mzaliwa wa Wales anayechezea klabu ya Portland Timbers ya Marekani aliyefunga dakika ya 15 tu.
    Lakini Misri ikazinduka kwa mabao ya winga wa Pyramids ya kwao, Mostafa Mohamed Zaky Abdelraouf ‘Ziko’ dakika ya 58, kiungo mshambuliaji wa Liverpool ya England na Nahodha, Mohamed Salah Hamed Mahrous Ghaly dakika ya 67 na winga wa Al Ahly ya nyumbani, Mahmoud Ahmed Ibrahim Hassan ‘Trézeguet’dakika ya 82.
    Msimamo wa Kundi G sasa ni Misri ipo kileleni kwa pointi zake nne ikifuatiwa na Iran na Ubelgiji zenye pointi mbili kila moja, wakati New Zealand yenye pointi moja inashika mkia.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAFARAO WA MISRI WAKIWASHA KOMBE LA DUNIA, WAICHAPA NEW ZEALAND 3-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top