• HABARI MPYA

    Wednesday, September 17, 2014

    DANNY WELBECK 'ALIVYOWAKERA' ARSENAL JANA...YEYE NA KIPA MARA TATU ANAKOSA MABAO

    MSHAMBULIAJI mpya wa Arsenal, Danny Welbeck jana alikuwa ana nafasi nzuri ya kuwa shujaa wa timu hiyo katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Borrusia Dortmund, lakini akashindwa kuitumia.
    Mchezaji huyo aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 16 kutoka kwa wapinzani, Manchester United jana alienedelea kupewa nafasi katika kikosi cha kwanza cha The Gunners na kocha Arsene Wenger akionyesha alimsajili kwa sababu alimuamini, lakini akashindwa kuwafurahisha mashabiki.

    Haamini macho yake; Mshambuliaji mpya wa Arsenal, Danny Welbeck akiwa amepiga magoti kwa masikitiko baada ya kupoteza nafasi nzuri ya kufunga kipindi cha kwanza jana

    Muingereza huyo jana alipata nafasi tatu nzuri za kuifungia Arsenal mabao kuanzia mapema kipindi cha kwanza, lakini zote akashindwa kuzitumia, The Gunners wakichapwa mabao 2-0 na Dortmund ugenini.
    Dhahiri Welbeck anahitaji kujiuliza mno baada ya mechi ya jana, kwani iwapo atarudia makosa aliyoyafanya katika mchezo huo, atajitengenezea mazingira ya kuondoka kwenye kikosi cha kwanza Gunners.
    Welbeck stumbles at the back post under pressure and misses a chance to give Arsenal the lead
    Mshambuliaji wa Arsenal, Danny Welbeck alipata nafasi nzuri ya kufunga hapa bao ambalo lingekuwa la kuongoza kwa Arsenal, lakini akakosa mpira ukimpita namna hii

    Nyingine hii; Danny Welbeck akianguka chini na kumshuhudia kipa wa Dortmund, Roman Weidenfeller akienda upande mwingine wa lango na mpira ukitoka nje baada ya kushindwa kuunganishia nyavuni
    Welbeck gets into another good shooting position late on but blazes the ball over the bar
    Na hii tena; Welbeck akapata nafasi nyingine tena, lakini akapiga juu ya lango
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DANNY WELBECK 'ALIVYOWAKERA' ARSENAL JANA...YEYE NA KIPA MARA TATU ANAKOSA MABAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top