• HABARI MPYA

    Saturday, December 01, 2012

    STARS YAMALIZANA NA SOMALIA LUGOGO LEO, ZANZIBAR NA MALAWI


    Kikosi cha Stars
    Na Mahmoud Zubeiry, Kampala
    MICHUANO ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge inatarajiwa kufikia tamati leo kwa hatua yake ya makudi, kwa mechi nne za Kundi B na C kupigwa kwenye viwanja tofauti mjini hapa.
    Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars watamenyana na Somalia kuanzia saa 8:00 mchana, kwenye Uwanja wa Lugogo na baadaye saa 10:00, Rwanda itacheza na Eritrea kwenye Uwanja huo huo.
    Sudan itamenyana na na Burundi kuanzia saa 8:00 mchana kwenye Uwanja wa Wankulunkulu na baadaye saa 10:00 jioni Malawi watamenyana na Zanzibar Wankulunkulu kwenye Uwanja huo huo.
    Mechi hizo, zimehamishwa kutoka Uwanja wa Mandela, Namboole, kutokana na Uwanja huo kuharibika na mvua zilizofululiza mjini na hapa na CECAFA imeamua kuupumzisha kwa muda.
    Kocha wa Kilimanjaro Stars, Kim Poulsen amefurahia kupona kwa beki Shomary Kapombe na ana matumaini ya kumtumia leo, ingawa kiungo Mwinyi Kazimoto ataendelea kujiuguza.
    Daktari wa Stars, Dk Mwanandi Mwankemwa, amesema mchezaji Kazimoto hataweza kucheza kwa kuwa bado anaendelea kupata nafuu kwa hivyo wamemshauri kocha ampumzishe katika mechi ya kesho.
    Stars pia itamkosa beki wake wa kushoto chaguo la kwanza, Amir Maftah ambaye ana kadi mbili za njano.
    Kocha huyo Mdenmark, amesema kwamba mechi ya leo itakuwa ni ya kufa na kupona na kikosi chake kiko tayari kukamilisha kazi.
    “Mechi hii ni sawa na kuwa na risasi moja na risasi hii unatakiwa kuitumia vizuri..ndio mtihani tunaokabiliwa nao katika mechi hii maana lazima tushinde ili tusinonge mbele katika mashindano haya,” alisema n akikosi chake kitapambana hadi dakika ya mwisho.
    Alisema ana imani na kikosi chake kwani wachezaji wote wana ari ya ushindi na kuendelea na mashindano kwani wameshaonesha kiwango kikubwa katika mechi mbili zilizopita huku Stars ikishinda mechi moja shidi ya Sudan na kufungwa nyingine na Burundi.
    “Katika mechi hii hakuna mchezo na nimeshawaambia wachezaji kabisa maana hapa ukifungwa unaondoka,” alisema.
    Meneja wa Bia ya Kilimanajro Premium Lager, wadhamini wa Stars, George Kavishe ametuma salamu muhimu hapa Kampala akisema kwamba mechi hii ni muhimu kwa Stars na kuwaomba Watanzania wanaoishi Uganda kujitokeza kwa wingi kuishangilia.
    “Vijana hawa wanahitaji sapoti kutoka kwa wadau wote  hasa katika mechi hii ya kesho itakayoamua kama Tanzania itafuzuu kuendelea au la….sisi tukiwa wadhamini wa timu tunafuatilia kwa karibu na tunawaomba Tanzania waishangilie na kuipa moyo timu yao,” alisema.
    Kikosi cha Stars kinachotarajiwa kuwa; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Issa Rashid, Shomari Kapombe, Kevin Yondan, Frank Domayo, Mrisho Ngassa, Amri Kiemba, John Bocco, Shaaban Nditi na Salum Abubakar.

    MSIMAMO KUNDI A:
                           P   W  D   L    GF GA GD Pts
    Uganda           3    3    0    0    6    0    6    9
    Kenya             3    2    0    1    4    2    2    6
    Ethiopia          3    1    0    2    2    3    -1  3
    Sudan Kusini  3    0    0    3    0    7    -7  0

    MSIMAMO KUNDI B:
                         P   W  D   L    GF GA GD Pts
    Burundi         2    2    0    0    6    1    5    6
    Tanzania       2    1    0    1    2    1    1    3
    Sudan           2    1    0    1    1    2    -1  3
    Somalia         2    0    0    2    1    6    -5  0

    MSIMAMO KUNDI C: 
                          P   W  D   L    GF GA GD Pts
    Zanzibar        2    1    1    0    2    1    1    4
    Rwanda         2    1    0    1    3    2    1    3
    Malawi           2    1    0    1    3    4    -1  3
    Eritrea           2    0    1    1    2    3    -1  1

    VIWANGO VYA UBORA FIFA
    NCHI                 NAFASI
    Uganda             86
    Malawi              101
    Ethiopia            102
    Sudan               102
    Rwanda             122
    Burundi             128
    Kenya                130
    Tanzania           134
    Zanzibar            134
    Somalia             193
    Eritrea               192
    Sudan Kusini     200
    (Viwango hivi vimetoka mwezi huu)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: STARS YAMALIZANA NA SOMALIA LUGOGO LEO, ZANZIBAR NA MALAWI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top