• HABARI MPYA

    Thursday, January 22, 2009

    ROY ALIKUWA 'PRODYUZA' WA KIPEKEE...


    Buriani Roy Bukuku, Bongo
    Fleva imepata pigo la kubwa…

    NA MAHMOUD ZUBEIRY
    “Hallow, Hi?”ilikuwa sauti nyororo ya mwanadada ikinisalimu, mara baada ya kufika kwenye kiji-soo (grocery) moja eneo la Keko Juu, Dar es Salaam.
    Wakati nimetuliza kumbukumbu na kumtazama kwa makini nikidadisi nilikuta naye wapi dada yule, akanipachika swali; “Kama umenisahau vile? Mimi naitwa Enika, tulikutana Habari Corporation, nilikuja kumtembelea Rashid Kejo, tunasoma naye TSJ (sasa IJMC)”.
    Naam hapo nilimtambua, wakati huo Enika alikuwa bado hajawa mwanamuziki maarufu. Wimbo wake `Baridi Kama Hili’ ndio kwanza unatoka mwishoni mwa mwaka 2003.
    Pembeni yake alikuwa ameketi kijana mmoja mrefu, mweusi na kw amwonekano ni mtaratibu hadi kwenye kuzungumza, Enika akanitambulisha: “Huyu anaitwa Roy, ni kaka yangu, yupo hapa G. Records,”.
    Njilifurahi kufahamiana na Roy, kwa muhtasari tangu ile akawa rafiki yangu hadi wa kutembeleana, alikuwa anakuja kwenye ghetto langu yeye na mdogo wake, G-Square kusikiliza nyimbo za Hip hop.
    Mimi ni mpenzi wa Hip hop, kadhalika Roy, alikuwa hivyo, hakika tulikuwa marafiki, watani, kwa kipindi kifupi.
    Wakati huo, Roy ndio anamtoa kijana Mr. Blue na wimbo wake Blue Blue, tangu hapo nikaanza kuandika kwa wingi habari G. Records.
    Nakumbuka wakati fulani wa sakata la Hip hop haiuzi, Roy alisimama kidete kutetea, akisstiza muziki huo unauza, lakini kwa msanii anayeufanya vizuri tu na si mbabaishaji.
    Roy alikuwa producer wa ukweli na mara nyingi alipenda kufanya kazi usiku, akiamini ni ndiop kipindi ambachoi akili yake inkuwa imetulia na kufanya kwa uhuru.
    Zaidi mchana alifanya marekebisho madogo na kusikiliza kazi alizofanya usiku uliopita, alipenda pombe, huo ni ukweli na tulikuwa tunakunywa naye, wakati mwingine hadi usiku wa manane.
    Wakati fulani Ruge Mutahaba wa Clouds FM aliwahi kutuita mimi na Roy: “Nyinyi wabishi mnaiop[enda Hip hop, njooni tuzungumze ili mjue kwa nini Hip hop haiuzi,”.
    Tulikwenda na Roy Rozana Bar, Buguruni ambako Clouds FM walikuwa wanafanya onyesho la madansa, Dance la Fiesta, tulibishana kwa hoja, mifano na hali halisi, ingawa hadi tunamaliza kikao, hakukuwa na suluhu, zaidi ya kila mmoja kushikilia msimamo wake.
    Roy alikuwa mtu mwenye kumheshimu yeyote, kufanya kazi na yeyote, alichokuwa akichukia yeye ni kitu kimoja tru, dharau, hakupenda dharau hata kidogo na wasanii wengi wenye majina waliokwenda G. Records kifua mbele, alikuwa akiwatoa nishai.
    Tulianza kupotezana na Roy baada ya mimi kuhama nyumbani Keko na kwenda kuanza maisha ya kujitegemea, mitaa ya Sinza. Baadaye naye alitibuana na Dj Gulu au G-Love na kutengana, hivyo kwenda kaunzisha studio yake mwenyewe, G2 ambayo ilipata umaarufu baada ya muda mfupi tu.
    Roy alikuwa producer gumzo na kipenzi cha wasanii wachanga, aliwainua wengi kama mmojawapo akiwa ni Matonya, Noorah mbali na Mr. Blue.
    Ukiketi kwenye kipindi cha muziki wa Bongo Fleva, nyimbo za G2 zilikuwa zinatawala. Wakati fulani, alimfunika kabisa P. Funk aliyekuwa anaongoza.
    Kwa sababu ya majukumu ya maisha, utu uzima tulizidi kupotezan na Roy na tukawa tunaonana mara moja moja, au wakti mwingine kurushiana salamu kwa njia ya simu.
    Lakini siku zote niliendelea kumheshimu Roy kwa sababu ya kazi yake, siyo muziki tu, hata matangazo yake ya biashara ni ya kiwango cha juu.
    Nakumbuka Roy aliniambia mwaka 1985 akiwa Uingereza alipokuwa anasoma alishiriki mashindano ya kupiga piano na kushinda na tangu hapo akaamua kuwa mtayarishaji wa muziki na matangazo ya Radio na TV kama kazi yake rasmi.
    Kabla ya G Records, Roy alikwishafanya kazi Sound-Crafters na aliwahi kurekodi wimbo wake mwenyewe, uliokwenda kwa jina la `Overnight’. Alishiriki pia kutayarisha albamu ya kwanza ya X- Plastaz.
    Sina nafasi ya kutosha kumuelezea zaidi Roy, aliyeaga dunia Jumatatu ya Oktoba 6, mwaka 2008 baada ya kusumbuliwa na maradhi ya mapafu, lakini kwa kiasi kikubwa alikuwa `bidhaa’ adimu kwenye anga za Bongo Fleva.
    Buriani Roy Bukuku, Mungu aiweke roho yake mahala pema peponi, Amin. Hakika Bongo Fleva imepata pigo la kubwa, naongea na wewe ndugu msomaji.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ROY ALIKUWA 'PRODYUZA' WA KIPEKEE... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top