• HABARI MPYA

  Alhamisi, Januari 22, 2009

  CHUJI APIGA BAO LA TATU LIGI KUU


  Kiungo wa Yanga, Athumani Iddi 'Chuji' (pichani), juzi alifunga bao lake la tatu msimu huu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tz Bara.

  Chuji aliyefunga mabao mawili kwenye michuano ya Challenge mjini Kampala Uganda, alifunga bao lake la tatu katika Ligi Kuu, kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, wakati timu yake, ikimenyana na Prisons.

  Hilo lilikuwa bao pekee lililoiwezesha Yanga kubeba pointi tatu muhimu katika harakati zake za kutetea ubingwa wake.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CHUJI APIGA BAO LA TATU LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top