• HABARI MPYA

        Friday, January 30, 2009

        MAMBO YAIVA COPA COCA COLA MWANZA

        VIONGOZI wa vyama vya soka vya wilaya za Mwanza wametakiwa kuchukua fomu za
        ushiriki wa mashindano ya Copa Coca Cola yatakayowahusisha vijana walio chini ya
        miaka 17.
        Katibu Mkuu wa Chama cha soka mkoani hapa (MZFA) Epaphra Swai alisema fomu hizo ziko tayari na kinachosubiriwa ni viongozi hao kufika ofisini kwake kuzichukua.
        “Ni vema wakaja mapema kuzichukua kwani muda unakwenda kwa kasi na tarehe ya mwisho ya kuzirudisha na Februari 5,” alisema.
        Fomu hizo zinatolewa bure kitendo kinacho maanisha kuwa timu nyingi zitashiriki na kuibua vipaji vipya.
        Aidha aliwataka viongozi wote kuhakikisha wanazingatia kanuni za mashindano hayo
        ambazo ni kuwasajili vijana walio chini ya umri wa miaka 17 na si vinginevyo.
        "Ni muhimu kanuni zilizowekwa zikazingatiwa na kuheshimiwa kwani ndio msingi wa
        mashindano hayo ambayo ni chachu ya kuendeleza soka la vijana," alisema Swai.
        Hayo yamekuja siku chache baada ya uzinduzi wa michuano hiyo uliofanyika katika viwanja vya kiwanda cha Coca Cola kilichoko Igoma jijini hapa.
        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: MAMBO YAIVA COPA COCA COLA MWANZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry