• HABARI MPYA

  Thursday, January 22, 2009

  BAYSER AREJEA NA MATAJI YAKE MTIBWA

  Mtibwa wakishangilia ubingwa wa kwanza tangu mwaka 2000 ilipotwaa Kombe la Ligi Kuu Bara  NAAM, Jamal Bayser amerejea rasmi kwenye shughuli za klabu yake, Mtibwa Sugar ya Turiani, Morogoro, baada ya kipindi cha miaka minne ya kuitumikia TFF (Shirikisho la Soka Tanzania) kama Mjumbe na badaaye Makamu wa Pili wa Rais.
  Akiwa TFF, Bayser alishuhudia Mtibwa ikiporomoka hadhi yake kwa kushindwa hata kushika nafasi tatu za juu kwenye Ligi Kuu, kama ilivyokuwa enzi yeye akiiongoza.
  Bayser aliiwezesha Mtibwa kutwaa ubingwa wa Bara kwa misimu miwili mfululizo 1999 na 2000, wakati miaka yote iliyofuata, Mtibwa ilikuwa haikosekani kwenye orodha ya timu tatu bora. Hata hivyo, tangu mwaka 2006, Mtibwa haijaweza kuwamo kwenye nafasi hizo. Lakini siku chache tu baada ya Bayser kurejea rasmi Mtibwa, timu hiyo iliweza kutwaa Kombe la Tusker, ikiitoa timu ngumu, Yanga na baadaye kwenye Nusu Fainali iliing'oa Tusker ya Kenya na kwenye fainali ikaifunga URA ya Uganda. Hizo ni ishara kwamba, Bayser amerejea na mataji yake Mtibwa. Simba na Yanga zikae chonjo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BAYSER AREJEA NA MATAJI YAKE MTIBWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top