• HABARI MPYA

  Monday, January 26, 2009

  POLISI ASHINDA RAV4 YA ZAIN SUMBAWANGA

  Daniel ole Njoolay: Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Daniel ole Njoolay (kushoto) akikabidhi ufunguo na mfano wa ufunguo kwa mshindi wa kumi wa zawadi ya gari aina ya Toyota RAV 4, Sweetbert Taga mjini Sumbawanga, mwishoni mwa wiki katika promosheni ya Endesha Ndoto 2 ya kampuni ya simu za mkononi ya Zain Tanzania

  KAMPUNI ya simu za mkononi ya Zain Tanzania Limited Jumapili ya Januari 25, mwaka huu ilikabidhi gari ya kumi, aina ya Toyota RAV 4 yenye thamani ya sh. milioni 45 kwa mshindi
  wa gari hilo mjini Sumbawanga.
  Sweetbert Damian Taga mwenye umri wa miaka 41, mkazi wa Sumbawanga
  alikabidhiwa gari hilo na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Daniel ole Njoolay
  katika hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika Sumbawanga na
  kushuhudiwa na watu mbalimbali wakiwemo ndugu wa mshidi. "Leo Zain Tanzania inayo furaha kukabidhi gari la kumi kwa mshindi wetu
  wa kumi katika promosheni ya Endesha Ndoto 2, na tunafurahi kwamba
  maisha ya mteja mwingine wa Zain yatabadilika na kuwa mazuri zaidi kwa
  sababu ya zawadi hii kubwa kutoka Zain.
  "Kama mnavyofahamu Zain imekuwa ikikabidhi gari moja kwa mtu mmoja kila
  mwezi tangu Januari mwaka jana katika promosheni ya Endesha Ndoto 2
  ikiwa ni sehemu ya programu yetu ya kurudisha kwa jamii na kuwashukuru
  wateja wa Zain kwa kuchagua Zain kuwa mtandao wao wa mawasiliano,”
  alisema Ofisa Uhusiano wa Zain Tanzania, Celine Njuju. Sweetbert ambaye ni askari Polisi, aliishukuru Zain kwa kuwajali wateja
  wake na akasema promosheni hiyo imewasaidia watu wengi. “Kwa kweli nina
  furaha isiyo kifani, jambo hili halijawahi kunitokea, nawashukuru sana
  Zain,” alisema. Sweetbert ni mteja wa kumi kunufaika na magari yaliyotolewa na Zain.
  Zain imetoa jumla ya magari 11 likiwemo aina ya Toyota Land Cruiser
  ambalo mshindi wake anatarajiwa kukabidhiwa hivi karibuni Dar es
  Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: POLISI ASHINDA RAV4 YA ZAIN SUMBAWANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top