• HABARI MPYA

  Jumamosi, Januari 24, 2009

  CHUJI: NINA HAMU KWELI NA HUYO ABOUTREIKA WENU
  KIUNGO wa klabu ya Yanga, Athumani Iddi ‘Chuji’, amesema kwamba pamoja na kuwa na matumaini ya kuitoa Etoile d’ Or Mironstsy ya Comoro karika Raundi ya Awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini wanawasubiri kwa hamu nyota wa Al Ahly (National) ya Misri ili wawaonyeshe kazi.
  “Najua watu wanatupigia hesabu kama sisi tumekwishatolewa na Al Ahly, lakini safari hii wataona kitu tofauti, mimi nakuambia, sasa hivi tuna akili kama wachezaji wa Magharibi, tunataka kucheza Ulaya,”alisema Chuji na kuongeza.
  “Ninamngoja kwa hamu sana huyo mtu anaitwa Mohamed Aboutreika, nataka nimuonyeshe kama mimi ninaijua soka zaidi yake, siyo hapa kwetu siyo kule kwao, sisi tutawaonyesha kazi hao Wamisri,”alitamba Chuji.
  Yanga itaanza kampeni yake ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kumenyana na Etoile d’ Or Mironstsy ya Comoro Jumamosi ijayo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kabla ya kurudiana wiki mbili baadaye.
  Ikifanikiwa kuitoa Etoile d’ Or Mironstsy, Yanga itakutana na mabingwa wa Afrika mara sita, Al Ahly.
  Kihistoria, Yanga haijawahi kuitoa timu yoyote ya Misri kwenye michuano ya Afrika zaidi ya kubebeshwa makapu ya mabao kila inapokwenda nchini humo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CHUJI: NINA HAMU KWELI NA HUYO ABOUTREIKA WENU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top