• HABARI MPYA

  Friday, January 30, 2009

  MIEMBENI YAWAFUATA WAZIMBABWE KIFUA MBELE

  Kipa wa Miembeni, Farouk Ramadhan

  KOCHA wa wawakilishi wa Zanzibar kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika timu ya Miembeni, Mkenya Tom Olaba amesema kutocheza mechi za kirafiki za kimataifa si kikwazo kwa timu yake kupata ushindi katika mchezo wa kesho dhidi ya Monomotapa ya Zimbabwe.
  Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kabla ya timu hiyo kuondoka kisiwani hapa, Olaba alisema wamejiandaa vizuri kuwakabili vijana hao wa Zimbabwe ingawa hawakucheza mechi yoyote ya kirafiki ya kimataifa.
  “Wachezaji wamejiandaa vizuri na wamefuata maelekezo na mafunzo yote kwa makini,” alisema.
  Katika michezo karibu 10 ya kujipima nguvu wachezaji wa Miembeni wameonekana kuzingatia mafunzo.
  Olaba aliwaomba Wazanzibar kuwaombea dua ili waweze kushinda.
  Timu hiyo iliondoka jana kwenda Zimbabwe ikiwa na msafara wa watu 22; wachezaji16 na viongozi sita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MIEMBENI YAWAFUATA WAZIMBABWE KIFUA MBELE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top