• HABARI MPYA

    Friday, January 23, 2009

    KILIMANJARO YALETA FARAJA SIMBA, YANGA




    Jumapili ya Agosti 18, mwaka jana, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia Bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager, ilisaini mkataba wa kuzidhamini klabu mbili kongwe nchini, Simba na Yanga zote za Dar es Salaam.
    Hafla ya utowaji zaini kwa mikataba hiyo, ilifanyika kwenye hopteli ya Movenpick, zamani Royal Palm mjini Dar es Salaam, ukihudhuriwa na pande zote za wahusika.
    Hakika udhamini huo wenye thamani ya Sh. Bilioni 3 kwa kila klabu katika kipindi cha miaka mitatu ni faraja kubwa kwa klabu hizo, ambazo ndiko mstari wa mbele kwenye soka ya Tanzania.
    Ukitazama orodha ya mabingwa wa soka Tanzania Bara, utagundua ni klabu hizo ambazo zimeongoza kutwaa taji hilo, zikifuatiwa kwa mbali na klabu za Mtibwa Sugar ya Morogoro, iliyotwaa mara mbili 1999 na 2000 kama ilivyo kwa Tukuyu Stars ya Mbeya (1985 na 1986), Coastal Union ya Tanga (1988), Mseto ya Morogoro (1975), zilizotwaa mara moja kila moja.
    Ni matumaini yetu, udhamini huu wa Kilimanjaro Lager ni faraja pia kwa mashabiki wa klabu hizo, ambao wanapenda kuona wachezaji wao wanacheza katika mazingira mazuri.
    Mchezo wa mpira wa miguu ni burudani inayounganisha maelfu ya watu wengi kwa wakati mmoja, hivyo Kilimanjaro Premium Lager imeungana na mamilioni ya mashabiki wa Simba na Yanga nchini kote kushangilia nao pamoja mafanikio ya klabu zao.
    Kwa sababu hiyo, Kilimanjaro Premium Lager inasema kwamba; kunywa Kilimanjaro, bia ya ushindi na shangilia timu yako ishinde.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    1 comments:

    Unknown said... January 24, 2009 at 1:26 AM

    ukiutai walioutoa kilimanjaro ni mkubwa kwa vilabu hivyo ni wakati sasa umefika kwa viongozi kuziacha tofauti zao ili kuweza kujipatia kila mwezi kile kitita cha mishahara kwa wachezaji na naomba isie ikatokeo mchezaji akalalamikia hajapata mshahara hapo lazima tutaonana wabaya,viongozi simba na yanga jamani chapeni kazi wakati ndio huu fanya kweli kwa maendeleo ya soka tanzania sio kwa maendeleo ya nyumbani kwako na familia yako.

    Item Reviewed: KILIMANJARO YALETA FARAJA SIMBA, YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top