• HABARI MPYA

  Jumatatu, Januari 26, 2009

  BANKA NJE MIEZI MIWILI SIMBA

  Banka wa pili kutoka kulia walioinama katika kikosi cha Simba mwaka 2007


  KIUNGO wa Simba, Mohamed Banka, atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi miwili baada ya kujitonesha nyonga katika mechi dhidi ya Villa wiki iliyopita.
  “Nina matatizo ya nyonga kwa kipindi kirefu sasa, kuna wakati nililazimika kupiga mpira kwa kulala (slide), nikajitonesha, hali iliyonifanya niwe vibaya zaidi. Kutokana na hali hiyo, sasa nalazimika kukaa bila kucheza hadi nitibiwe na kupona kabisa.
  “Sidhani kama nitacheza tena katika mechi hizi kabla ya mapumziko ya kupisha fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani. Naweza kusema nitakaa kitu kama miezi miwili hivi hadi niwe safi, ndiyo nianze tena mazoezi,” alisema mchezaji huyo.
  Banka, aliyeanza kipindi cha kwanza katika mechi hiyo akiwa miongoni mwa viungo wanne waliokuwa na jukumu la kuunganisha timu, akiwa pamoja na Jabir Aziz, Nico Nyagawa na Ramadhan Chombo ‘Redondo’ alitolewa kabla ya kumalizika kwa dakika 45 za kwanza kutokana na kutoonyesha kandanda safi.
  Alisema atapata matibabu yake katika hospitali ya Aga Khan ambako wachezaji wote wa Simba wanatibiwa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BANKA NJE MIEZI MIWILI SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top