• HABARI MPYA

  Friday, January 30, 2009

  VODACOM KUTUMIA MIL 65 KUIBUA VIPAJI MWANZA

  KAMPUNI ya simu za mkononi ya Vodacom kupitia programu yake ya Cheza na Vodacom imetoa Sh. milioni 65 kwa ajili ya kuibua vipaji vya michezo katika mikoa sita ya kanda ya ziwa.
  Pamoja na kuibua vipaji malengo mengine ni kuziunganisha jamii za watu wa kanda ya ziwa, kwa kuishi kwa amani na upendo kupitia michezo mbalimbali.
  Akizungumza na BINGWA, Mratibu wa Michezo hiyo, Emmanuel Seni alisema kwa sasa mashindano ya Cheza na Vodacom yanaendelea mkoani Shinyanga na baadaye yatafanyika mkoani Kagera, Mara na kumalizikia jijini Mwanza Machi mwaka huu.
  Aliitaja michezo ambayo imedhaminiwa na Vodacom kuwa ni mpira wa miguu, pete, wavu, kupiga kasia, mbio za baiskeli, bao na pool table.
  Alisema mashindano hayo yalizinduliwa rasmi Januari 7, mwaka huu, Igunga, Tabora na baadaye yalifanyika Nzega, Nkinga, Mwisi, Ndala, Puge, Kigwa, Tabora Hotel, Imalakaseko, Skonge na Urambo.
  “Wananchi wanatakiwa kujitokeza kushiriki katika michezo hii kwani inamanufaa mengi kwao ikiwamo kujijengea afya bora, kukuza ujirani mwema na kujishindia zawadi mbalimbali kutoka kampuni Vodacom kama vile, mipira, fulana, seti za jezi za Vodacom zenye thamani ya Sh. 250,000 na fedha taslimu,” alisema.
  Mikoa sita ambayo mashindano hayo yatafanyika ni Tabora, Shinyanga, Mwanza, Kagera, Mara na Kigoma.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: VODACOM KUTUMIA MIL 65 KUIBUA VIPAJI MWANZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top