• HABARI MPYA

  Ijumaa, Januari 30, 2009

  MABONDIA MORO WATAMBA KUSHINDA

  Francis Cheka atakayepigana na Matumla pambano kuu


  BAADHI ya mabondia watakaotetea mikanda yao katika michezo ya utangulizi kabla ya pambano kati ya bingwa wa ngumi za kulipwa nchini Francis Cheka na Rashid Matumla, wametamba kuwasambaratisha wapinzania wao katika dakika za awali za mapambano yao.
  Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti wakiwa mazoezini katika ukumbi wa
  Mandela mjini hapa, mabondia hao walisema mwaka huu ni wa kurudisha heshima ya
  ushindi katika michezo mkoani hapa.
  Deo Njiku, anayetarajia kuvaana na Maliki Kinyogoli, alisema kutokana na maandalizi aliyoyafanya ana uhakika wa kumtoa mpinzani wake dakika za awali na kufuta mawazo kuwa yeye ni njia.
  Katika mchezo huo utakaokuwa wa kuwania ubingwa wa taifa uzito wa kilo 63, Njiku alisema anataka kuwadhihirishia mashabiki na wapenzi wa ngumi mkoani hapa kuwa anafaa kushikilia mkanda huo.
  Akizungumzia maendeleo ya maandalizi ya mchezo huo, kocha wa ngumi wa klabu ya Mandela, Boma Kilangi alisema mabondia wote wanaendelea vema na hakuna majeruhi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MABONDIA MORO WATAMBA KUSHINDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top