• HABARI MPYA

  Thursday, January 22, 2009

  UDHAMINI WA KILIMANJARO WAZIDI KUZING'ARISHA SIMBA, YANGA LIGI KUU VODACOM

  Simba, Yanga zapeta...

  SIMBA na Yanga za Dar es Salaam, zinazodhaminiwa na Kampuni ya Bia
  Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager, juzi
  ziliendela kung'ara katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya
  kuibuka na ushindi kwenye viwanja tofauti.Simba iliibuka na ushindi wa 2-0 kdhidi ya Villa Squad ya Kinondoni,
  mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, wakati Yanga
  iliibwaga Prisons 1-0 kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.Kwa ushindi huo Simba imeendelea kujisogeza juu katika jitihada zake
  za kuwasogelea watani wao wa jadi, Yanga ambao msimu huu wamerejea
  kasi yao ya mwaka 1998, walipoweza kutwaa ubingwa kabla ya mechi
  tatu za Ligi.Simba sasa imetimiza pointi 20 baada ya kucheza mechi 13, hivyo
  kupanda hadi nafasi ya nne, wakati Villa inayoshika nafasi ya pili kutoka
  mkiani, imebaki na pointi zake 11.Yanga nayo imezidi kupaa, sasa ikiwa inaongoza kwa tofauti ya pointi
  13, kwani kwa ushindi wa juzi imetimiza pointi 36.Mabao ya SImba juzi yalitiwa kimiani na Mussa Hassan 'Mgosi' katika dakika ya dakika 22 na Ulimboka Mwakingwe (PICHANI) dakika 55.Yanga nayo ilipata bao lake pekee kwenye Uwanja wa Sokoine mjini
  Mbeya, kupitia kiungo wake hodari, Athumani Iddi 'Chuji' dakika ya 76.Simba: Ally Mustafa 'Barthez', Nasoro Said 'Choiro', Juma Jabu, Kelvin
  Yondan, Juma Nyoso, Mohamed Banka, Nico Nyagawa, Jabir Aziz, Mussa
  Mgosi, Ulimboka Mwakingwe na Ramadhani Chombo 'Redondo'.Villa Squad: Mustafa Mbarouk, Godfrey Taita, Yusuph Gogo, Athumani Kibarati, Abdallah Said, George Kavila, Mussa Nampaka, Andrew Carlos, Hemed Shaaban, Laurent Mugia na Ally Kolwa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: UDHAMINI WA KILIMANJARO WAZIDI KUZING'ARISHA SIMBA, YANGA LIGI KUU VODACOM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top