• HABARI MPYA

  Jumatano, Januari 21, 2009

  HATIMAYE HISTORIA YAANDIKWA MAREKANI

  Barack Obama
  HATIMAYE historia mpya imeandikwa duniani, baada ya mtu wa kwanza mwenye asili ya Afrikas, Barack Hussein Obama kuapishwa Januari 20, mwaka 2009 kuwa rais wa 44 wa Marekani.
  Baada ya kuapishwa, Obama ambaye baba yake alikuwa raia wa Kenya, alitoa hotuba akitoa wito kwa Wamarekani kuwa na imani imara na kuungana kama kitu kimoja ili kukabiliana na changamoto za aina mbalimbali.
  Rais Obama alisema Marekani inakabiliwa na matatizo mbalimbali yanayosababishwa na vita na msukosuko wa fedha, hivyo si rahisi kushinda changamoto hizo kubwa kwa haraka. Aliwataka wananchi wa Marekani wasawazishe misimamo yao, kujitahidi kubeba wajibu, na kutoa mchango wao katika kukabiliana na msukosuko na kustawisha uchumi wa taifa.
  Rais Obama alisema Marekani itawajibika kuondoa jeshi lake kutoka Iraq, kujitahidi kulinda amani nchini Afghanistan; kutokomeza tishio la nyuklia; na kuendelea kupambana na ugaidi. Alisema serikali mpya ya Marekani itatafuta njia mpya ya kuendeleza uhusiano kati yake na nchi za kiislamu chini ya msingi wa kuheshimiana na kunufaishana, na Marekani itatoa misaada mingi zaidi kwa nchi maskini.
  Siku hiyo baraza la juu la Marekani lilitoa orodha ya kwanza ya mawaziri wa serikali ya awamu mpya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: HATIMAYE HISTORIA YAANDIKWA MAREKANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top