TIMU ya Azam FC imefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayodhaminiwa na Benki ya CRDB baada ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya waliokuwa mabingwa watetezi, Yanga SC jioni ya leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Katika mchezo huo ambao mabao yote yalifungwa kwa vichwa – waliofungia Azam FC ni kiungo Himid Mao Mkami dakika ya 28, beki Lameck Eliasi Lawi dakika ya 85 na mshambuliaji Mkongo, Jephte Kitambala Bola dakika ya 112.
Katika mchezo huo uliodumu kwa dakika 120 kufuatia dakika 90 za awali kumalizika timu hizo zikiwa zimefungana 2-2, Azam FC ilicheza pungufu tangu dakika ya 70 kufuatia beki wake, Yoro Mamadou Diaby raia wa Mali kutolewa kwa kadi nyekundu.
Azam FC sasa itakutana na Simba SC katika Fainali baadaye mwezi huu baada ya wekundu wa Msimbazi jana kuitoa Coastal Union ya Tanga kwa kuichapa 4-0, mabao ya Libasse Guèye dakika ya 20, Nickson Clement Kibabage dakika ya 55, Rushine De Reuck dakika ya 75 na Clatous Chota Chama dakika ya 79 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.



.png)
0 comments:
Post a Comment