• HABARI MPYA

    Sunday, August 12, 2012

    PREVIEW NGAO YA JAMII CHELSEA NA MAN CITY


    MECHI YA NGAO YA JAMII
    Agosti 12, 2012 (Saa 9:30 jioni)
    Villa Park — Birmingham
    Refa:‬ K. Friend‎



    CHELSEA

    Cech
    Ivanovic, Cahill, Terry, Cole
    Lampard, Mikel, Meireles
    Ramires, Torres, Hazard

    MANCHESTER CITY

      
    HartZabaleta, K Toure, Lescott, Kolarov
    Y Toure, De Jong
    A Johnson, Tevez, Nasri
    Aguero

    Juan Mata anatarajiwa kukosekana Chelsea leo, kufuatia kushiriki kwake Michezo ya Olimpiki, hivyo Roberto Di Matteo anaweza kutumia mfumo wa 4-3-3 katika safu ya kiungo Raul Meireles akiungana na Frank Lampard na John Obi Mikel.

    Ramires na Eden Hazard wanaweza kumsapoti Fernando Torres katika safu ya ushambuliaji, wakati Mtaliano huyo anaweza kuamua kati ya Gary Cahill na David Luiz amuanzishe nani katika safu ya ulinzi. Marko Marin ataikosa mechi hiyo kutokana na maumivu ya nyama.

    Roberto Mancini ana wakati mgumu wa kuamua nani amuanzishe kwenye kikosi cha kwanza. 

    Viwango vya wachezaji wengi waliocheza Euro 2012 kama Samir Nasri na Nigel de Jong vinatia shaka, wakati Vincent Kompany ni majeruhi, ingawa anaweza kuchezeshwa hivyo hivyo, na inawezekana pia Kolo Toure akaanza katika beki ya kati.

    David Silva na Mario Balotelli wote walifika fainali na timu zao katika Euro nchini Poland na Ukraine na wote wanatarajiwa kuanzia benchi.

    Yaya Toure, Sergio Aguero na Carlos Tevez wote wako sawa sawa na wanaweza kuanza kwenye 11 wa watakaotangulizwa uwanjani, lakini Gareth Barry ni majeruhi na Micah Richards hatacheza baada ya kuiwakilisha Uingereza kwenye Olimpiki.

    JE WAJUA?

    • Manchester City ilifungwa mabao 3-2 na wapinzani wao Manchester United katika mechi ya Ngao ya Jamii mwaka jana, lakini imetwaa taji hilo mara tatu – katika miaka ya 1937, 1968 na 1972.
    • Villa Park, nyumbani kwa Aston Villa, ni Uwanja wa unaochukua nafasi ya mechi hiyo, badala ya Wembley ambao unatumika kwa Michezo ya Olimpiki Jijini London.
    • Mechi hiyo itachezwa nje ya Uwanja wa Taifa – (Wembley wa England au Millennium wa Wales – kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1973 ilipochezwa kwenye Uwanja wa zamani wa City, Maine Road.
    • Maine Road umetumika kwa mechi za Ngao mara tano, wakati mechi hiyo imechezwa mara nyingi zaidi kwenye Uwanja wa Chelsea, Stamford Bridge kuliko Uwanja mwingine wowote.
    • Chelsea iliifunga City nyumbani katika Ligi Kuu msimu uliopita, lakini ilifungwa nayo kwenye Uwanja wa Etihad kwa kipigo sawa na walichowapa wapinzani wao hao, mabao 2-1.
    • Kwa ujumla, The Blues wameshinda mechi 55 dhidi ya City walioshinda 43, na mechi 36 baina ya timu hizo zilimalizika kwa sare.
    • Chelsea imetwaa Ngao mara nne, tatu kati ya hizo katika milenia mpya, mwaka 2000, 2005 na 2009. Pia walitwaa 1955.
    • Hii itakuwa mechi ya kwanza ya mashindano kwa Roberto Di Matteo, kama Kocha Mkuu rasmi, akiwa ni Mtaliano wa nne kushika wadhifa huo Stamford Bridge, baada ya Carlo Ancelotti, Claudio Ranieri na Gianluca Vialli.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PREVIEW NGAO YA JAMII CHELSEA NA MAN CITY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top