• HABARI MPYA

    Friday, September 28, 2018

    MBAO FC YAICHOMOLEA COASTAL MKWAKWANI NA KUREJEA KILELENI LIGI KUU

    Na Mariam Maumba, TANGA
    TIMU ya Mbao FC imerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya sare ya ugenini ya 1-1 na wenyei, Coastal Union Uwanja wa CCM Mkwakwani mjini Tanga. 
    Coastal Union ambayo imeendelea kukosa huduma ya mchezaji wake mpya, Ally Kiba ilitangulia kwa bao la Ayoub Lyanga dakika ya 31 kabla ya Said Khamis kuisawazishia Mbao FC dakika ya 50.  
    Na kwa sare hiyo, Mbao FC inafikisha pointi 14 baada ya kucheza mechi saba, ikiishushia nafasi ya pili Mtibwa Sugar yenye poinyi 13 za mechi saba pia. 

    Mbao FC imerejea kileleni Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya sare ya ugenini ya 1-1 na Coastal Union Mkwakwani leo

    Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Kagera Sugar imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Ndanda FC ya Mtwara katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliofanyika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
    Mabao ya Kagera Sugar ya kocha Mecky Mexime leo yamefungwa na Ramadhani Kapera mawili, dakika za 47 na 86 na lingine Japhet Makalai dakika ya 52, wakati la Ndanda FC limefungwa na Mohamed Manzi dakika ya 59.
    Kwa ushindi huo, Kagera Sugar inafikisha pointi 10 baada ya kucheza mechi sita, ikishinda mbili na kutoa sare nne, wakati Ndanda FC inabaki na pointi zake saba baada ya kucheza mechi saba.
    Nayo Stand United imelazimishwa sare ya bila kufungana na Tanzania Prisons ya Mbeya Uwanja wa CCM kambarage mjin Shinyanga. Stand United inafikisha pointi 11 baada ya kucheza mechi nane na Prisons inafikisha pointi saba katika mechi ya nane.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MBAO FC YAICHOMOLEA COASTAL MKWAKWANI NA KUREJEA KILELENI LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top