• HABARI MPYA

    Thursday, September 20, 2018

    SPORTPESA YAZINDUA 'DILI' LA WATU KUJISHINDIA BAJAJI MPYA KILA SIKU

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KAMPUNI ya kubashiri michezo nchini ya SportPesa leo imezindua rasmi promosheni ya kuinua maisha kiuchumi SHINDA ZAIDI NA SPORTPESA itakayodumu kwa siku 100 ambapo mshindi ataweza kujishindia BAJAJ RE mpya, pesa taslimu au vyote kwa pamoja. Promosheni ya SHINDA ZAIDI NA SPORTPESA inaanza leo Alhamisi 20 Septemba 2018. 
    Akizungumza kwenye uzinduzi wa promosheni hiyo leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa, Tarimba Abbas amesema kuwa hii ni mara ya pili kwa kampuni hiyo kuendesha promosheni kama kwa wateja wake. ‘Mwaka jana tuliendesha promosheni kama hii – Shinda na SportPesa ambapo tulitoa bajaj 100 kwa washindi wetu. Washindi walitoka kwenye mikoa yote 23 ya Tanzania na waliweza kubadilisha maisha kwa kujiongezea kipato cha kila siku kupitia bajaj ambazo wengi wao waliweza kuzitumia kwa ajili ya biashara. Nia yetu sisi SportPesa ni kuendelea kuinua na kubadilisha maisha ya Watanzania kupitia michezo," alisema Tarimba.
    Zoezi la ufunguzi rasmi wa promosheni ukiongoza na Mkurugenzi Mtendaji wa SportPesa Tanzania Bwana Pavel Slavkov na Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti  Ndugu Tarimba Abbas

    Hizi ndizo Bajaji ambazo watu watajishindia kila siku kupitia SportPesa


    Kwa kupitia Shinda Zaidi na SportPesa, tutaweza kubadilisha maisha ya Watanzania kwa kupitia kushinda Bajaj pamoja na zawadi zingine kwa muda wa siku 100. Ninayo furaha kuwa SportPesa imekuwa ikibadilisha maisha ya Watanzania kiuchumi kwa kupitia michezo. Tangu Mei 2017 ambapo kampuni ya SportPesa ilianza kufanya shughuli zake hapa nchini, kampuni imeweza kutoa TZS 26.5 bilioni kama zawadi kwa Watanzania wanaobashiri kupitia SportPesa, aliongeza Tarimba.
    Kupitia promosheni ya Shinda Zaidi na SportPesa, kama kampuni tutaweza kubadili maisha ya watanzania kupitia Bajaj RE na zawadi nyingine ambazo zitatolewa kwa kipindi cha siku zisizopungua 100. Tunaridhika na kujivunia jinsi kampuni yetu inavyobadili na kuinua kiuchumi maisha ya watanzania kupitia michezo. Tangu Mei 2017 ambapo SportPesa ilianzishwa rasmi nchini Tanzania, jumla ya Milioni 26.5 bilioni zimezawadiwa kwa washindi wanaocheza na kampuni yetu.
     Promosheni ya Shinda na SportPesa ambayo tuliendesha mwaka jana ilikuwa na mafanikio makubwa na ndio sababu iliyotufanya kuja na promosheni hii ya Shinda Zaidi na SportPesa. Naomba kutoa rai yangu kwa wateja wetu kutumia hii fursa hii na kubadilisha maisha yao kwa kushinda zawadi mbali mbali. Hii ni promosheni kwa wateja wetu na kila mmoja anayo nafasi ya kuwa mshindi, alisema Tarimba.
    Tarimba alisema kuwa kampuni ya SportPesa ikiwekeza kwenye kubadilisha maisha ya Watanzania kwa kudhamini na kuwekeza kwenye michezo hapa nchini. Ni kwa kupitia SportPesa Super Cup ambapo timu ya Everton kutoka Uingereza iliweza kufanya ziara na kucheza mechi ya ushindani kwenye uwanja wa Taifa hapa Dar es Salaam kwa mara ya kwanza katika historia. Tumekuwa pia tukidhamini timu mbali mbali za soka na hii imekuwa ni chachu kwa timu hizo na pia imeongeza ushindani kwenye ligi Kuu hapa Tanzania. Vile vile, mwaka jana SportPesa iliweza kutumia TZS 1.4 bilion kwenye kukarabati uwanja wa Taifa ikiwa ni juhudi za kuunga mkono serikali kwenye kuendeleza michezo hapa nchini. Hii imekuwa ni kutokana na ushirikiano kutoka kwa wateja wetu, wadau pamoja na serikali ya Tanzania na nachukua fursa hii kutoa shukrani za dhati kila mtu.
    Kwa upande wake, Meneja Uhusiano SportPesa Sabrina Msuya alisema kuwa ili kushiriki kwenye promosheni ya Shinda Zaidi na SportPesa na kushinda Bajaj RE mpya mteja atatakiwa kubashiri kwa kuanzia TZS1000.
     “Kama bado hujawahi kucheza na SportPesa basi hakikisha unapiga *150*87# KUWEKA UBASHIRI wako mara nyingi zaidi ili uweze kuingia kwenye droo, alisema Msuya.
    Msuya alisema kuwa promosheni iliyopita ilifikia mikoa 23 ya Tanzania na kwamba kila aliweka ubashiri wake alipata nafasi ya kujishindia pesa taslimu, jezi, na safari ya kwenda Uingereza au Bajaj. Kwa TZS1000, unaweza kubadilisha maisha yako kwa kupitia SportPesa, aliongeza Msuya.
    Akiongea kwenye uzinduzi huo, Venkatesh. K- Business, Mkurugenzi wa Submean Auto Ltd ambao ndio wasambazaji wa Bajaj RE hapa Tanzania alisema, ‘Sisi Sunbeam Limited tunatoa waranti wa miezi 12 kwa Bajaj RE 4S ili kuonyesha imani yetu kwa bidhaa zetu. Natoa rai yangu kwa Watanzania kubashiri kupitia SportPesa na kuwa washindi, aliongeza.
    Ikiwa imeashisha 2014, SportPesa ni kampuni ya kubashiri michezo ambayo anafanya kazi zake Kenya, Tanzania, Afrika Kusini na UK ambapo inafanya kazi kwa kushirikiana na TGP Europe. Ndio kampuni ya kubashiri michezo inayoongoza Afrika ambao inatoa bashiri zaidi ya 500 kila siku kwa wateja wake na wapenzi wa mpira kujishindia zawadi kem kem na pia inadhamini klabu za ligi kuu ya Kenya na Tanzania.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SPORTPESA YAZINDUA 'DILI' LA WATU KUJISHINDIA BAJAJI MPYA KILA SIKU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top