• HABARI MPYA

    Sunday, September 30, 2018

    KIKOSI CHA SIMBA SC MECHI NA WATANI HIKI HAPA; OKWI, CHAMA NA KAGERE WOTE WANAANZA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KOCHA Mbelgiji wa Simba SC, Patrick J Aussems amewaanzisha kwa pamoja washambuliaji Emmanuel Okwi na Meddie Kagera kwa ajili ya mchezo dhidi ya mahasimu, Simba SC jioni ya leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
    Watani wa jadi, Simba na Yanga watamenyana Uwanja wa Taifa kuanzia Saa 11:00 jioni katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, ambao utahudhuriwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai.
    Na kwa mchezo huo, kikosi cha Simba SC tayari kipo hewani na langoni anaendelea kusimama ‘Tanzania One’, Aishi Manula.

    Kikosi kamili cha Simba SC leo ni; Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Erasto Nyoni, Pascal Wawa, James Kotei, Jonas Mkude, Cletus Chama, Meddie Kagere, Emmanuel Okwi na Shiza Kichuya.
    Katika benchi Aussems pamoja na wasaidizi wake; atakaa na wachezaji akiba akina Deo Mushi ‘Dida’, Paul Bukaba, Asante Kwasi, Said Ndemla, Mohammed ‘Mo’ Ibrahim, Nicholas Gyan na Adam Salamba.  
    Ikumbukwe mechi hiyo itachezeshwa na refa Jeonisya Rukyaa kutoka Kagera akisaidiwa na Ferdinand Chacha wa Mwanza na Mohamed Mkono wa Dar es Salaam pembezoni mwa Uwanja na Mezani atakuwepo Elly Sasii.
    Jeonesia Rukyaa, refa wa Kagera tayari ana uzoefu wa kupuliza kipyenga katika michezo ya watani wa jadi, baada ya awali kuchezesha mechi mbili.
    Kwanza ilikuwa Desemba 13, mwaka 2014 mechi ya Mtani Jembe, Simba SC wakishinda 2-0, mabao ya Awadh Juma na Elias Maguri na ya pili Februari 20, mwaka 2016 Yanga SC wakishinda 2-0, mabao ya Donald Ngoma na Amissi Tambwe. 
    Mchezo wa kesho utakuwa wa pili kuzikutanisha timu hizo mwaka huu, baada ya Aprili 29 Simba SC kushinda 1-0, bao pekee la Erasto Edward Nyoni dakika ya 37, mechi ya marudiano ya msimu uliopita wa Ligi Kuu. 
    Mechi ya kwanza ya msimu huo, timu hizo zilitoka sare ya 1-1 Oktoba 28 Uwanja wa Taifa Simba wakitangulia kwa bao la Shiza Kichuya dakika ya 57, kabla ya Obrey Chirwa kuisawazishia Yanga dakika ya 60.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIKOSI CHA SIMBA SC MECHI NA WATANI HIKI HAPA; OKWI, CHAMA NA KAGERE WOTE WANAANZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top