• HABARI MPYA

    Thursday, September 27, 2018

    AMUNIKE ‘AWAKAUSHIA’ NYONI NA KICHUYA TAIFA STARS, AWACHUKUA NGALEMA NA KIHIMBWA KIKOSI CHA KUIVAA CAPE VERDE

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KOCHA Mnigeria wa Tanzania, Emmanuel Amunike hajawajumuisha beki Erasto Nyoni na viungo Shiza Kichuya wa Simba na Ibrahim Ajib wa Yanga katika kikosi chake cha wachezaji 30 kuelekea mechi mbili za kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya Cape Verde.
    Taifa Stars watakuwa wageni wa Cape Verde katika mchezo wa Kundi L kufuzu AFCON Oktoba 12 mjini Praia kabla ya kurejea Dar es Salaa kwa mchezo wa marudiano na wapinzani wao hao Oktoba 16.
    Na Amunike leo ametaja kikosi cha awali cha wachezaji 30 kwa ajili ya mechi hizo, akiwaweka kando nyota kadhaa, wakiwemo Nyoni na Kichuya. 
    Shiza Kichuya (kulia) amekuwa mchezaji muhimu wa Taifa Stars kabla ya ujio wa Emmanuel Amunike 

    Kwa kiasi kikubwa ameita wachezaji waliomsaidia kupata sare ya ugenini Septemba 8 mjini Kampala na Uganda, ingizo jipya wakiwa ni Shomari Kapombe, Jonas Mkude wa Simba SC, Abdallah Kheri wa Azam FC, Andrew Vincent ‘Dante’ na Feisal Salum wote wa Yanga SC.
    Kikosi kamili cha Taifa Stars kilichotajwa leo ni makipa; Aishi Manula (Simba SC), Beno Kakolanya (Yanga SC) na Mohamed Abdulahman (JKT Tanzania).
    Mabeki; Hassan Kessy (Nkana FC/Zambia), Shomari Kapombe (Simba SC), Salum Kimenya (Tanzania Prisons), Gardiel Michael (Yanga SC), Paulo Ngalema (Lipuli FC), Ally Sonso (Lipuli FC), Aggrey Morris (Azam FC), David Mwantika (Azam FC), Abdallah Kheri (Azam FC), Kelvin Yondani (Yanga SC), Andrew Vicent (Yanga SC) na Abdi Banda (Baroka FC).
    Viungo ni Himid Mao (Petrojet/Misri), Simon Msuva (Difaa Hassan El –Jadida/Morocco), Mudathir Yahya (Yanga SC), Frank Domayo (Azam FC), Jonas Mkude (Simba SC), Feisal Salum (Yanga SC), Salum Kihimbwa (Mtibwa Sugar) na Farid Mussa (CD Tenerife/Hispania).
    Washambuliaji; Mbwana Samatta (Nahodha, KRC Genk/Ubelgiji), Thomas Ulimwemgu (Al Hilal/Sudan), John Bocco (Simba SC), Yahya Zayd (Azam), Kelvin Sabato (Mtibwa Sugar), Rashid Mandawa (BDF XI/Botswana) na Shaaban Iddi Chilunda (CD Tenerife/Hispania).
    Amunike anasaidiwa na Hemed Suleiman ‘Morocco’ na Mnigeria mwenzake, Emeka Amadi, wakati Mtunza Vifaa ni Ally Ruvu na Madaktari Richard Yomba na Gilbert Kigadya.
    Tanzania inashika nafasi ya tatu katika Kundi L ikiwa na pointi mbili tu baada ya sare zote katika mechi zake mbili za mwanzo, 1-1 na Lesotho nyumbani mwaka jana na 0-0 na Uganda ugenini mapema mwezi huu.
    Uganda wanaendelea kuongoza Kundi hilo kwa pointi zao nne, wakifuatiwa na Lesotho mbili sawa na Tanzania na mabao mawili ya kufunga, wakati Cape Verde wanashika mkia kwa pointi yao moja. 
    Kihistoria Tanzania imecheza fainali moja tu za AFCON, mwaka 1980 nchini Nigeria, tena enzi hizo bado zinajulikana kama Fainali za kombe la Mataifa Huru ya Afrika. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AMUNIKE ‘AWAKAUSHIA’ NYONI NA KICHUYA TAIFA STARS, AWACHUKUA NGALEMA NA KIHIMBWA KIKOSI CHA KUIVAA CAPE VERDE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top