Umony akiwa na ramadhan Sarpei, mmoja wa viongozi wa timu ya Sudan mjini hapa |
Na Mahmoud Zubeiry,
Kampala
MSHAMBULIAJI
wa Uganda, Brian Umony amekwishasema yuko tayari kujiunga na klabu ya Simba ya
Dar es Salaam, lakini kabla Wekundu hao wa Msimbazi hawajachukua hatua yoyote,
El Merreikh ya Sudan imetuma mwakilishi wake hapa azungumze na mchezaji huyo.
Habari
ambazo BIN ZUBEIRY imezipata mjini hapa zimesema kwamba, Merreikh
inayosuka upya kikosi chake baada ya kukosa ubingwa wa Sudan, imetuma
mwakilishi wake hapa afanye mazungumzo na Umony, aliyekoswakoswa kidogo tu na
Simba mwaka 2009, alipokuwa KCC ya hapa.
Mwandishi
mmoja wa habari wa Sudan, ameiambia BIN ZUBEIRY jana katika hoteli ya Silver Springs
mjini hapa kwamba, tayari mwakilishi huyo wa Merreikh yuko hapa kwa kazi hiyo.
Aidha,
Mwandishi huyo amesema mwakilishi huyo wa Merreikh atatazama vipaji zaidi
kuanzia hatua ya Robo Fainali kwa ajili ya kupendekeza wachezaji wapya wa
kusajiliwa na klabu hiyo.
Mwandishi
huyo alisema tayari Merreikh pia imekubaliana biashara na Yanga juu ya kiungo
Haruna Niyonzima, Nahodha wa Rwanda katika Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki
na Kati, CECAFA Tusker Challenge.
Mwishoni mwa
wiki, akizungumza na BIN ZUBEIRY mjini hapa baada ya
kuiongoza Uganda kuifunga Sudan Kusini maao 4-0 katika mechi ya mwisho ya Kundi
A, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na kati, CECAFA Tusker Challenge, Umony
alisema Simba kama wanamtaka wamfuate haraka wamalizane.
Brian
amerejea nyumbani Uganda na kujiunga na Express baada ya kumaliza mkataba wake,
Becamex Binh Duong F.C. ya Vietnam.
Mwaka 2009,
baada ya Simba kuzidiwa kete na SuperSport United ya Afrika Kusini, ikamsajili
Emmanuel Okwi aliyekuwa SC Villa wakati huo.
Umony
aliichezea Supersport United hadi 2010 alipohamia University of Pretoria ya
Afrika Kusini pia hadi mwaka 2011 alipohamia Portland Timbers ya Marekani kwa
mkopo na mwaka huu akatua Becamex Binh Duong F.C. Brian anang’ara katika Kombe
la Challenge, hadi sasa ana mabao matatu.