Okwi katika Challenge ya mwaka huu |
Na Mahmoud Zubeiry,
Kampala
AZAM FC
wametuma mwakilishi wao hapa kufuatilia wachezaji katika mashindano ya Kombe la
Mataifa ya Afrika Masahariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge yanayoendelea
mjini hapa tangu Novemba 24, hadi Desemba 8, mwaka huu.
Mwakilishi
huyo alitua hapa jana na kuanzia leo ataanza kufanya kilichomleta mjini hapa.
Rasmi Azam
inakuwa klabu ya pili kutuma mwakilishi wake hapa baada ya El Merreikh ya
Sudan.
Mapema
mwanzoni mwa mashindano haya, ilielezwa wawakilishi wa Simba, Yanga na Coastal
Union watakuja pia hapa kutazama vipaji vya kuongeza katika klabu zao, lakini
hadi jana hakukuwa na taarifa za mwakilishi yoyote wa klabu hizo kufika hapa.
Mkurugenzi
wa Ufundi wa Coastal Union, Nassor Bin Slum ilielezwa atatua leo sawa na Seif
Ahmad ‘Seif Magari’, Abdallah Ahmad Bin Kleb wa Yanga na Geoffrey Nyange
‘Kaburu’ wa Simba.
Kiongozi wa
zamani wa Simba SC, Alhaj Juma Nkamia, ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Kondoa
Kaskazini yeye tayari yupo hapa kwa wiki nzima, lakini ameletwa na mapenzi yake
kwa timu yake ya taifa.
Kuna
wasiwasi, mmoja wa wachezaji ambao Azam imekuja kuwatazama huku ni mshambuliaji
wa Simba SC, Mganda Emmanuel Okwi ambaye inadaiwa mkataba wake umemalizika,
ingawa klabu yake imesema unaisha Mei mwakani.