• HABARI MPYA

    Saturday, June 20, 2026

    'WACHEZAJI WA GHANA' WAISAIDIA UHOLANZI KUICHAPA SWEDEN 5-1 KOMBE LA DUNIA


    TIMU ya Uholanzi imeibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Sweden katika mchezo wa Kundi F Fainali za Kombe la Dunia usiku huu Uwanja wa NRG, Houston, Texas, Marekani.
    Mabao ya Uholanzi ‘Orange’ yamefungwa na washambuliaji wanaocheza England watupu, Brian Ebenezer Adjei Brobbey wa Sunderland, mawili dakika ya tano na 17, Cody Mathès Gakpo wa Liverpool dakika ya 47 na 54, wote wana asili ya Ghana – huku lingine likifungwa na winga wa West Ham United, Crysencio Jilbert Sylverio Cirro Summerville mwenye asili ya Suriname dakika ya 89.
    Bao pekee la Sweden ambayo mechi ya kwanza nayo ilishinda 5-1 dhidi ya Tunisia – limefungwa na mshambuliaji wa Newcastle United ya England pia, Anthony David Junior dakika ya 59.
    Mechi nyingine ya kundi hilo itafuatia Saa 1:00 Asubuhi kati ya Tunisia na Japan Uwanja wa BBVA, Guadalupe, Nuevo León nchini Mexico.
    Kwa ushindi huo, Uholanzi inafikisha pointi nne na kupanda kileleni mwa Kundi F ikiizidi pointi moja Sweden baada ya timu hizo zote kucheza mechi mbili – zikifuatiwa na Japan yenye pointi moja na Tunisia ambayo haijavuna pointi bado kufuatia mechi za kwanza.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: 'WACHEZAJI WA GHANA' WAISAIDIA UHOLANZI KUICHAPA SWEDEN 5-1 KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top