• HABARI MPYA

    Saturday, June 20, 2026

    GALARZA APIGA BONGE LA BAO PARAGUAY YAICHAPA UTURUKI 1-0 MAREKANI


    TIMU ya Paraguay imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Uturuki katika mchezo wa Kundi D Fainali za Kombe la Dunia Asubuhi ya leo Uwanja wa Levi's, Santa Clara, California, Marekani.
    Bao pekee la Paraguay limefungwa na kiungo Matías Galarza Fonda anayecheza kwa mkopo Atlanta United ya Marekani kutoka River Plate ya Argentina dakika ya pili tu ya mchezo huo.
    Mchezo mwingine wa kundi hilo usiku wa jana, wenyeji, Marekani waliichapa Australia 2-0 mabao ya mabeki, Cameron Robert Burgess wa  Swansea City ya England mzaliwa wa Scotland aliyejifunga dakika ya 11 na Alexander Michael Freeman wa Villarreal ya Hispania aliyefunga dakika ya 43 Uwanja wa Lumen Field, Seattle, Washington.
    Kwa matokeo hayo, msimamo wa Kundi D sasa ni Marekani inaongoza kwa pointi zake sita ikifuatiwa na Australia pointi tatu sawa na Paraguay zikizidiana wastani wa mabao, wakati Uturuki ambayo haina pointi inashika mkia.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: GALARZA APIGA BONGE LA BAO PARAGUAY YAICHAPA UTURUKI 1-0 MAREKANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top