• HABARI MPYA

    Friday, September 12, 2014

    PIGO LINGINE UKUTA WA MAN UNITED, PHIL JOSEN NJE WIKI TATU

    PIGO lingine katika safu ya ulinzi ya Manchester United, baada ya Phil Jones kuumia akiichezea England dhidi ya Uswisi Jumatatu mechi ya kuwania tiketi ya Euro 2016 na sasa atatakiwa kuw anje kwa wikihadi tatu.
    Beki huyo wa Manchester United amekuwa chini ya uangalizi wa timu ya madaktari ya klabu tangu amerejea kutoka Basle, ambako alicheza kwa dakika 77 kabla ya kumpisha Phil Jagielka.
    Kulikuwa kuna wasiwasi kwamba Jones anaweza kuwa nje kwa mwezi mmoja, lakini vipimo vimeonyesha anaweza kuwa nje kwa wiki mbili hadi tatu. 
    Phil Jones atakuwa nje kwa wiki mbili hadi tatu baada ya kuumia nyama akiichezea England
    Phile Jones was part of the defence that earned England a 2-0 victory over Switzerland in Basle
    Phile Jones alikuwemo kwenye kikosi kilichoshinda 2-0 dhidi ya Uswisi mjini Basle

    MECHI AMBAZO JONES ATAZIKOSA MAN UNITED 

    14 Septemba             QPR (Nyumbani)
    21 Septemba             Leicester (Ugenini)
    27 Septemba             West Ham (Nyumbani) 
    Jones wazi sasa atakosa mechi za Manchester United dhidi ya QPR Uwanja wa Old Trafford Jumapili ambako wachezaji wanne wapya wanawexa kuanza kuitumikia klabu hiyo.
    Radamel Falcao na Daley Blind walitambulishwa jana kama wachezaji wapya wa klabu hiyo na wanaweza kuungana na wenzao wengine wapya, Luke Shaw na Marcos Rojo.
    Kocha Louis van Gaal bado anasotea ushindi wa kwanza katika Ligi Kuu England, baada ya mwanzo mbaya ambao imeshuhudiwa akiambulia pointi mbili tu huku akitolewa na timu ndogo MK Dons katika Kombe la Ligi, maarufu Capital One Cup. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PIGO LINGINE UKUTA WA MAN UNITED, PHIL JOSEN NJE WIKI TATU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top