MSHAMBULIAJI Radamel Falcao anatumai kwamba Manchester United itamsajili moja kwa moja atakapomaliza Mkataba wake wa mkopo wa Pauni Milioni 6, kwani anataka kudumu Old Trafford kwa miaka mingi kutengeneza historia.
Mshambuliaji huyo wa Colombia ametambulishwa rasmi leo sambamba na kiungo aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 14, Daley Blind baada ya kufanya mazoezi yake ya kwanza na timu ya Louis van Gaal.
United ina nafasi ya kumnunua moja kwa moja Falcao kutoka Monaco msimu ujao kwa dau la Pauni Milioni 52 baada ya kukubali mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 mshahara wa Pauni 280,000 kwa wiki msimu huu.
Nataka kubaki miaka mingi: Mshambuliaji wa Monaco, Radamel Falcao amesema anataka kubaki kwa miaka mini Manchester United
Akizungumza kwa kuchanganya lugha Kiingereza na Kispanyola, Falcao alisema: "Natumai kubaki miaka mingi Manchester United na kutengeneza historia katika klabu hii. Wakati nilipokuwa FC Porto na Atletico Madrid daima nilitaka kukuza kiwango kwa ndoto za kucheza timu kubwa kama hii. Sasa nataka kubaki hapa kwa miaka mingi,"amesema.
Mapinduzi ya Wekundu: Louis van Gaal (katikati) akijiandaa kuwatambulisha wachezaji wapya Radamel Falcao (kushoto) na Daley Blind (kulia) Uwanja wa Old Trafford
0 comments:
Post a Comment