Na Asha Said, DAR ES SALAAM
RAIS wa bendi ya Mashuja ‘Wana Kibega’, Charles Gabriel 'Chalz Baba' amesema amewataka wapenzi wa bendi hiyo wajitokeze kwa wingi katika maonesho yao matatu ya utambulisho wa albamu yao ya Ushamba mzigo.
Akizungumza na Waandashi wa Habari Dar es Salaam leo, Chalz Baba alisema, baada ya kwenda mikoa mbalimbali, sasa wanamalizia Dar es Salaam kwa shoo tatu ili kuhitimisha maonyesho 30 ambayo walipanga kufanya.
Alisema shoo ya kwanza Dar es Salaam itakuwa Ijumaa hii katika ukumbi wa Ten Roung zamani Millennium Business Park, Jumamosi katika ukumbi wa Bwalo la Magereza na Jumapili kumalizia katika ukumbi wa Peace of Mine uliopo Tabata.
“Tumezunguka sana, mikoa mbalimbali hapa nchini, na tumefarijika kuwaona mashabiki na wadau wetu wanaotufanya Mashujaa tuzidi kuwepo mpaka sasa, hivyo basi katika hizi shoo zitaenda sambamba na uzinduzi wa albam yetu ya Ushamba Mzigo ambayo tunaiingiza rasmi sokoni ikiwa ya muziki na video,”alisema.
Naye Meneja wa bendi hiyo, Martine Sospeter alisema, ziara yao ilienda sawa, ambapo yeye alikuwa mkuu wa msafara, kwani kikubwa zaidi wanamshukuru Mungu walikwenda na kurejea salama.
Meneja wa mauzo wa Bavaria, Jestas Kyolike, akiwataka wadau na mashabiki wa bendi hiyo, kuendelea kutumia kinywaji hicho kwani wao wataendelea kuwaunga mkono Mashujaa bendi katika safari yao ya mafanikio zaidi.

![]() |
Charles Baba kusshoto akizungumza na Waandishi wa Habari |

0 comments:
Post a Comment