Na Ameir Khalid, ZANZIBAR
WAKONGWE wa soka Zanzibar Malindi SC, leo wameshindwa kuzikamata mashua za wanamaji wa KMKM kwa kukubali kipigo cha mabao 2-1 katika mechi ya ligi kuu iliyochezwa uwanja wa Amaan jioni hii.
KMKM ambao ndio wanaoshikilia ubingwa wa ligi hiyo inayodhaminiwa na kinywaji cha Grand Malt, walianza kuzifumania nyavu za wapinzani wao mapema sekunde ya 48 kwa bao lilifungwa na mshambuliaji wake hatari Mudrik Muhibu.
Wachezaji wa KMKM wakishangiria bao la pili kwa staili ya ndege wanaoruka.
Muhibu alifunga bao hilo baada ya kazi nzuri ya kuwaramba chenga walinzi wa Malindi na kupiga shuti lililomshinda kipa Said Omar.
Bao hilo lilidumu hadi mapumziko na KMKM wakazidi kutawala kipindi cha pili na kuwafunika wachezaji wa Malindi, huku wakiongozwa na mtoto wa mchezaji wa zamani wa timu hiyo Ibrahim Kapenta, Maulid.
Maulid Kapenda akawainua mashabiki wa KMKM kwa kupachika bao la pili katika dakika ya 62.
Mchezaji Haji wa Haji aliipatia Malindi bao la kufutia machozi katika dakika ya 84 baada ya kuwatoroka mabeki wa KMKM na kuachia shuti zuri lililompita kipa kipa Mudathir Khamis.
Na katika uwanja wa Gombani kisiwani Pemba ambao leo ulishuhudia mechi ya kwanza tangu kuanza kwa ligi hiyo, maafande wa Polisi na wana mitulinga wa Hard Rock walishindwa kutambiana baada ya kutoka sare tasa.
Kesho katika uwanja wa Amaan, Mtende Rangers watawavaa wachunga wafungwa, Mafunzo huku wanagenzi waliopanda msimu huu Shaba SC kutoka wilaya ndogo ya Kojani wakipimana ubavu na timu ya Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) katika uwanja wa Gombani Pemba.

0 comments:
Post a Comment