BONDIA wa uzito wa juu, Anthony Joshua ameendeleza wimbi la ushindi baada ya kumpiga kwa Knockout (KO) raundi ya tatu Konstantin Airich usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Manchester Arena, England.
Mbabe huyo mwenye umri wa miaka 24 anayefananishwa Lennox Lewis alijifua kwa kupigana kwa siku 10 mazoezini na mfalme wa uzito wa juu, Wladimir Klitschko kujiandaa na pambano hilo.
Lewis mpya; Bondia Anthony Joshua akiinua mikono juu kushangilia ushindi wake ukumbi wa Manchester Arena |
Hilo linakuwa pambano la nane mfululizo kushinda bila kupoteza hata moja tangu ahamie kwenye ndondi za kulipwa, hivyo kuendeleza vyema safari yake ya kuwa bondia mkubwa duniani.
Bingwa huyo wa uzito wa juu wa Olimpiki baada ya pambano hilo, alisema; "Natumia muda wangu kufanya vitu. Nafurahia hii, kupata uzoefu wa kiwanfo hiki,"amesema.
0 comments:
Post a Comment