BEKI wa kulia wa Brazil, Maicon ametemwa kwenye kikosi cha timu ya taifa katakana na utovu wa nidhamu.
Maicon, beki wa zamani wa Manchester City, alicheza mechi yote ya kwanza baada ya kocha Carlos Dunga kurejea , Brazil ikishinda 1-0 dhidi ya Colombia mjini Miami Jumamosi.
Pamoja na hayo, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33, ambaye amechezea Brazil mechi 76, ameenguliwa katika kikosi kinachojiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Ecuador mjini New York Jumanne.
Mzoefu: Maicon, akipambana na Radamel Falcao Jumamosi, kabla ya kutemwa na kocha Dunga kwa utovu wa nidhamu
Maicon alijiunga na Manchester City mwaka 2012 akitokea Inter Milan kwa Pauni Milioni 3, lakini akashindwa kuendana na mfumo wa maisha katika Ligi Kuu ya Engand.
Alirejea tena Serie A akijiunga na Roma msimu uliopita baada ya kucheza mechi tisa tu kwa mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England.
0 comments:
Post a Comment