KIGOGO wa soka duniani, Sepp Blatter amethibitisha atasimama kugombea urais wa FIFA kwa mara ya tano mwakani.
Blatter amekuwa akitarajiwa sana kugombea tena licha ya mwaka 2011 kusema hii itakuwa awamu yake ya mwisho na sasa amethibitisha atafanya hivyo.
Inafuatia Rais wa UEFA, Michel Platini kutangaza mwezi uliopita kwamba hatagombea uongozi FIFA.
Nje ya mbio: Rais wa UEFA, Michel Platini hatashindana na Blatter kuwania nafasi hiyo ya juu katika ulimwengu wa soka
Blatter amesema ataitambulisha rasmi Kamati Kuu ya FIFA juu ya mipango yake katika kikao cha Septemba 25 na 26.
Babu huyo mwenye umri wa miaka 78 amesema hayo katika mahojiano ya video ya Soccerex katika Mkutano mjini Manchester: "Nitaithibitishia Kamati Kuu. ni suala la heshima kusema hivyo, kisha kwenye familia ya soka, ndiyo nitakuwa tayari. Nitakuwa mgombea. Unaona mpango haujakamilika. Na mpango wangu haujaisha,"amesema.
0 comments:
Post a Comment