KIUNGO Cesc Fabregas amesema kwamba daima atajihisi kama Mshika Bunduki - licha ya uhamisho wa Pauni Milioni 30 kwa wapinzani wa Arsenal Jijini London, Chelsea msimu huu.
Kiungo huyo wa Hispania ameingia vizuri Stamford Bridge, akichangia mno mafanikio ya sasa ya timu hiyo, akiwa amekwishatoa pasi nne za mabao hadi sasa msimu huu.
Na baada ya kuhama Barcelona akiwa bado kinda- Fabregas alijiunga na Arsenal, kisha akarejea Camp Nou kabla ya kuhamia Chelsea.
Arsenal damu: kiungo Cesc Fabregas pamoja na kutua Chelsea kwa Pauni Milioni 30 msimu huu akitokea Barcelona, amesema ana mapenzi na Arsenal
"Daima nitajihisi mshika bunduki na nifahamu kwamba nitarudi [Uwanja wa Emirates] na ninahisi huo utakuwa ni wakati maluum, lakini nimejifunga,"amesema Fabregas.
"Kumbuka kwamba nimecheza fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Barcelona. Ninaapa kwako, kwamba ningefanya kila lililowezekana kushinda mechi ingawa nilikuwa Barcelona tangu mdogo.
"Hivyo unafahamu kwamba, ninapocheza dhidi ya Arsenal nafahamu ninacheza na nani, akina nani ni wachezaji wenzangu na mani nitamtetea, nafahamu kwamba mashabiki wa Arsenal wataelewa; Sina shaka,".
Kiungo huyo alikuwa anatakiwa na klabu kadhaa England zilizoshindana na Chelsea kuwania saini yake, lakini mwishowe akaangukia The Blues.



.png)
0 comments:
Post a Comment