UJERUMANI jana imeshinda mabao 2-1 dhidi ya Scotland katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Euro, lakini habari kubwa ilikuwa ni Ikechi Anya aliyefunga bao la kufutia machozi dhidi ya mabingwa wa dunia.
Anya alifunga dakika ya 66 mjini Dortmund ambalo lilikuwa la kusawazisha wakati huo, baada ya Thomas Muller kutangulia kuwafungia wenyeji kabla ya baadaye kufunga la ushindi.
Kiungo huyo wa Watford mwenye umri wa miaka 26, amefurahi mno baada ya kufunga kiasi cha kulia, akisema hakuamini kama ameweza kumfunga kipa bora duniani Manuel Neuer, na akasema hawezi kufanya hivyo kwenye mashindano ya FIFA.
Kilio cha furaha: Anya akilia wakati wa kushangilia bao lake jana
Kiungo huyo wa Watford akimtungua kipa bora duniani
Hiki ndicho alichposti kwenye Twitter Anya baada ya mechi
"Nimemtungua Manuel Neuer!!! Wowwww siwezi kufanya hive hata katika FIFA," ameposti Anya mwenye asili ya Nigeria, aliyeamua kuchezea Scotland soka ya kimataifa.
0 comments:
Post a Comment