KIUNGO David Silva amewatuliza presha mashabiki wa Chelsea kwa kusema mchezaji mwenzake wa timu ya taifa ya Hispania, Diego Costa hajaumia sana nyama.
Mpachika mabao huyo wa Hispania alipata matatizo hayo akiwa na timu yake hiyo ya taifa kwenye maandalizi ya mchezo wa kuwania kucheza Fainali za Euro 2016 dhidi ya Macedonia.
Costa amefunga mabao manne katika mechi zake tatu za mwanzo Ligi Kuu ya England, akiashiria mwanzo mzuri wa maisha yake mapya Stamford Bridge, lakini wasiwasi ulianza kabla ya mechi na Everton mwishoni mwa wiki, kwamba ametonesha maumivu aliyoyapata mwishoni mwa msimu uliopita alipokuwa Atletico Madrid.
Mtu muhimu: Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho atatumaini Diego Costa anaweza kucheza mechi ijayo
Pamoja na hayo, mchezaji mwenzake wa Hispania anayechezea Manchester City, David Silva hammini kama maumivu hayo ni makubwa na ana matumaini kwamba Costa atakuwa fiti kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Swansea Uwanja wa Stamford Bridge wikiendi ijayo, pamoja na dhidi ya timu ya Silva, Manchester City wiki moja baadaye.
"Nimemuona Costa anaendelea vizuri na nimezungumza naye. Hana maumivu makali," amesema Silva.
Costa alirejea London jana kwa vipimo juu ya maumivu yake ingawa taarifa rasmi juu ya hali yake bado haijatolewa.
0 comments:
Post a Comment