Na Dina Ismail, DAR ES SALAAM
KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Athumani Iddi Athumani ‘Chuji’ ameenda kuanza maisha mapya ya soka nje ya Afrika baada ya kupata ofa ya kujiunga na Oman Club ya Oman.
Chuji alitarajiwa kuondoka Dar es Salaam jioni hii kwenda kujiunga na klabu hiyo kubwa barani Asia, ambayo inacheza Ligi Kuu ya Oman.
Hatua ya kiungo huyo kuhamia Asia, inafuatia kugoma kuongeza mkataba na klabu yake, Yanga SC ya Dar es Salaam msimu uliopita baada ya kutofautiana na aliyekuwa kocha Msaidizi wa timu hiyo, Charles Boniface Mkwasa.
Baada ya kushindana na Yanga SC, Chuji alitaka kujiunga na Azam FC, ambako hata hivyo baadhi ya viongozi walikataa mchezaji huyo kusajiliwa wakidai ana rekodi ya utovu wa nidhamu.
Kufuatia kukwama mipango ya kujiunga na Azam FC, Chuji aliendelea kujifua mwenyewe huku wakala wake akimtafutia timu nje- hatimaye amefanikiwa kuhamishia soka yake bara Asia.
Kabla ya Yanga SC, Chuji, mtoto wa mchezaji wa zamani wa CDA ya Dodoma, Iddi Athumani ‘Pajero’ alichezea Polisi Dodoma na Simba SC ya Dar es Salaam pia.

![]() |
Maisha nje ya Afrika; Athumani Iddi 'Chuji' amekwenda kujiunga na Oman Club |
Baada ya kushindana na Yanga SC, Chuji alitaka kujiunga na Azam FC, ambako hata hivyo baadhi ya viongozi walikataa mchezaji huyo kusajiliwa wakidai ana rekodi ya utovu wa nidhamu.
Kufuatia kukwama mipango ya kujiunga na Azam FC, Chuji aliendelea kujifua mwenyewe huku wakala wake akimtafutia timu nje- hatimaye amefanikiwa kuhamishia soka yake bara Asia.
Kabla ya Yanga SC, Chuji, mtoto wa mchezaji wa zamani wa CDA ya Dodoma, Iddi Athumani ‘Pajero’ alichezea Polisi Dodoma na Simba SC ya Dar es Salaam pia.
0 comments:
Post a Comment