• HABARI MPYA

    Monday, September 08, 2014

    BILA RONALDO, URENO YAPIGWA 1-0 NA ALBANIA KUFUZU EURO 2-16

    URENO ikicheza bila nyota wake Cristiano Ronaldo imefungwa bao 1-0 na Albania katika mchezo wa kuwania kufuzu kwenye Fainali za Euro 2016. 
    Baada ya kuvurunda Kombe la Dunia Juni mwaka huu nchini Brazil, Ureno imekutana na pigo lingine kwa bao pekee la Bekim Balaj kipindi cha pili. 
    Matokeo ya mechi nyingine za kufuzu Euro 2016 jana, Gibraltar imefungwa 7-0 nyumbani na Poland, Faroe Islands imefungwa 3- 1 na Finland, Ugiriki imegungwa 1-0 na Romania, Ujerumani imeifunga 2-1 Scotland, Georgia imefungwa 2-1 na Jamhuri ya Ireland, Denmark imeifunga 2 - 1 Armenia na Hungary imefungwa 2-1 na Ireland Kaskazini.
    Aibu: Mshambuliaji wa Albania, Bekim Balaj (katikati) akishangilia baada ya kuifungia timu yake bao pekee dhidi ya Ureno mjini Aveiro
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BILA RONALDO, URENO YAPIGWA 1-0 NA ALBANIA KUFUZU EURO 2-16 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top