• HABARI MPYA

    Monday, September 08, 2014

    MULLER AING'ARISHA UJERUMANI KUFUZU EURO 2016

    MABAO mawili ya Thomas Muller yameipa Ujerumani ushindi wa 2-1 dhidi ya Scotland katika mchezo wa kufuzu fainali za Euro 2016.
    Mshambuliaji huyo wa Bayern Munich aling'ara mno katika mchezo huo na kuendeleza mafanikio ya Ujerumani baada ya kutwaa Kombe la Dunia akifunga dakika za 18 na 70, wakati bao la Scotland limefungwa na Ikechi Anya dakika ya 66.
    Nyota huyo alifunga mabao yake ya 24 na 25 katika mechi 58 dhidi ya Scotland iliyomaliza na wachezaji 10 baada ya Charlie Mulgrew kutolewa kwa kadi nyekundu dakika za majeruhi.
    Mtaalamu: Thomas Muller akiifungia Ujerumani jana dhidi ya Scotland 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MULLER AING'ARISHA UJERUMANI KUFUZU EURO 2016 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top