KLABU ya Arsenal imepiga picha ya kikosi chake kizima kipya wachezaji wakiwa na Kombe kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2005, The Gunners wakiwa wamepozi na mataji ya FA na Ngao ya Jamii.
Picha hiyo inahusisha wachezaji wapya waliosajiliwa msimu huu, sambamba na makinda waliopandishwa kutoka timu ya vijana.
Danny Welbeck, aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 16 kutoka Manchester United katika siku ya mwisho ya kufungwa kwa pazia la usajili amesimama katikati ya wachezaji wenzake wapya Calum Chambers na beki kinda wa pembeni Hector Bellerin mstari wa pili, wakati Alexis Sanchez ni mchezaji pekee mpya aliyekaa mstari wa mbele.
Wachezaji wapya wa Arsenal, Mathieu Debuchy, Calum Chambers, David Ospina, Danny Welbeck na Alexis Sanchez
Wachezaji wapya Sanchez na Welbeck wakiwa na kiungo mwenyeji kikosini Jack Wilshere (katikati) wakati wa upigaji picha
0 comments:
Post a Comment