Wachezaji wa Uganda
wakimpongeza Geoffrey Kizito (anayetazama kamera amekumbatiana na Kiiza), baada
ya kufunga bao kwanza dakika ya nne dhidi ya Ethiopia katika Robo Fainali ya
Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge kwenye Uwanja
wa Mandela, Namboole mjini Kampala. Uganda ilishinda 2-0 bao lingine likifungwa
na Robert Ssentongo dakika ya 60 na kwa ushindi huo, Uganda itamenyana na
Tanzania Bara katika Nusu Fainali Alhamisi usiku, mchezo ambao utatanguliwa na
Nusu Fainali nyingine kati ya Kenya na Zanzibar.
|