YANGA SC wanataka kwenda Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo (CAS) kupinga maamuzi ya Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kumtangaza mchezaji Emmanuel Okwi ni huru.
Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria ya Yanga SC, Sam Mapande amezungumza hayo na Waandishi wa Habari juzi, siku moja tu baada ya Kamati hiyo ya TFF kufikia maamuzi hayo.
Mapande amesema kwamba hawajaridhishwa na maamuzi hayo ambayo yanakinzana na shitaka zima la mchezaji huyo.
Amesema Kamati hiyo ya TFF imeamua sakata la Okwi kinyume cha malalamiko yao, kwani hakukuwa na lalamiko la mchezaji huyo wa Uganda kuhusiana na malipo ya fedha zake za usajili.
Alisema inashangaza Kamati hiyo ya TFF iliamua kusikiliza kesi ambayo haikuwa mbele yao na kutoa maamuzi ambayo hata wao wameshangazwa nayo.
“Kwanza kesi yenyewe ilikuwa haijamalizika, walituambia tuwasilishe vielelezo kuhusiana na kitendo cha mchezaji huyo kufanya mazungumzo na klabu ya Misri, lakini cha kushangaza maamuzi yametolewa, hili limetushangaza sana,” alisema Mapande.
Alisema kuwa mazingira yalikuwa yameandaliwa kuibeba Simba na Okwi kwani hata malalamiko yao kwa Simba hayakusikilizwa. “Malalamiko yetu yalikuwa wazi kabisa, yapo kimaandishi, hatukuwahi kulalamikiwa, suala la fedha za usajili la Okwi limetoka wapi, kama lilikuwepo, mbona hatujajulishwa kimaandishi kama utaratibu ulivyo,” alisema.
Mapande pia, alilalamikia Kamati hiyo kumruhusu Mjumbe wake, Zacharia Hans Pope ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Simba kuwemo katika kikao hicho ni kinyume na taratibu za FIFA kupitia kifungu namba 19 kinachoeleza mgongano wa kimaslahi.
Kwa kukumbushia, historia ya Yanga SC na Okwi inaanzia Desemba mwaka jana, walipomsajili mchezaji huyo kwa dau la dola za Kimarekani 100,000 na mchezaji huyo akapewa fedha nusu kwanza, akiahidiwa kumaliziwa Januari.
Hata hivyo, kufika Januari, mchezaji huyo hakumaliziwa fedha zake, lakini akaipa muda klabu hiyo hadi Machi alipoamua kususa ili kushinikiza madai yake.
Katikati yalifuatia mazungumzo baina ya Yanga SC na Okwi ambayo vyombo vya habari vilikuwa vikiyaripoti na wakati fulani, Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yussuf Manji aliwahi kusema mchezaji huyo atabaki kwa kuwa kuna mazungumzo yanaendelea.
Juni 27, mwaka huu, Yanga SC waliandika barua TFF kumlalamikia mchezaji huyo na mwishowe wakaomba; “With that said, we request your good office to nullify our agreement with Mr Emmanuel Arnold Okwi and oblig him to refund us the Sinning Fee paid to him as advance and in good faith, refund Yanga salaries wrlongly collected by him and make the player pay damages to the tune of USD 200,000 to the club due for the loss of income and good will for not retaining the Premier League Championship and Mark our Agreement with him as not consummated,”
Bila shaka baada ya ukimya wa TFF kutojibu barua hiyo ya Juni 27, Yanga wakaandika barua nyingne Agosti 25 ambayo malalamiko dhidi ya mchezaji yaliongezeka.
Walimlalamikia kuingia kwenye mazungumzo na klabu Wadi Degla ya Misri akiwa bado ana Mkataba na klabu na kwa sababu hiyo wakaomba;
“With that said, we would like to request your good office to do the following; Mark Yanga’s agreement with Mr Okwi to at the prerogative of Yanga to terminate without any need of compensation to Mr Okwi,”.
Katika kikao cha Kamati Jumapili, Kamati kilijadili mgogoro wa mchezaji na klabu- kikagundua kwamba tangu Januari mkataba baina ya pande hizo mbili ulikwishavunjika.
Nani ameuvunja? Yanga SC kwa kitendo cha kutomlipa mchezaji haki zake kwa mujibu wa makubaliano ya kwenye Mkataba.
Kitu ambacho kilikuwa kinasubiriwa hapa ni mamlaka za soka kuhalalisha uvunjikaji wa ndoa hiyo- na ndicho kilichofanyika Jumapili.
Kwa maana hiyo, hata madai ya Yanga SC katika barua yao ya Agosti 25 kwamba mchezaji huyo alifanya mazungumzo na klabu ya Misri, hayana uzito kwa kuwa hata kama alifanya hivyo, ni miezi kadhaa baada ya kuvunjika kwa mkataba wake na klabu ya Tanzania.
Hoja kwamba kesi yao Yanga SC haikusikilizwa ni kichekesho- kwa sababu mgogoro uliowasilishwa mbele ya Kamati ni wa Kimkataba na kilichofanywa na Kamati hiyo ni kuupitia Mkataba hadi kugundua hayo.
Hoja kwamba, Hans Poppe ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili na Mjumbe wa Kamati ya Sheria Maadili na Hadhi za Wachezaji ya TFF hivyo hakupaswa kushiriki kikao kuepuka mgongano wa kimaslahi- kwanza haibadilishi ukweli wowote juu ya hukumu ya Kamati.
Lakini pili, vyanzo vinasema kikao hakikufikia kwenye kupiga kura kufanya maamuzi, bali wanasheria wa pande mbili walishindana kwa hoja na wa Yanga SC akashindwa.
Yanga SC wanatakiwa kukubali walipokosea na kuachana na suala la Okwi, ili wasipoteze muda zaidi na gharama pia.
Yanga SC wanatakiwa kujifunza kutokana na makosa waliyoyafanya kwa Okwi- ili wasirudie kwa wachezaji wengine.
Leo yanazungumzwa ya Okwi- lakini Yanga SC ilijiruhusu vipi kiungo Frank Domayo hadi akamaliza Mkataba kabisa na kwenda Azam FC kama mchezaji huru?
Didier Kavumbangu walisema hawakuwa na nia ya kuendelea naye akaenda Azam FC pia kama mchezji huru na Mwenyekiti, Yussuf Manji akasema atasajili wakali wengine, tumewaona akina Geilson Santana Santos ‘Jaja’ na Andrey Countiho. Lakini vipi Domayo?
Na je, ni wachezaji wangapi katika kikosi cha sasa Yanga SC nao makubaliano ya kwenye mikataba yao hayazingatiwi, lakini hawajachukua hatua yoyote?
Yanga SC kwa sasa ndiyo wanajua siri za mikataba yao na wachezaji wao, ila wanapaswa kutambua katika dunia ya leo mambo yamebadilika mno, hivyo wachukue tahadhari yasije kujirudia ya Okwi.
Tunafahamu siasa za Simba na Yanga, wanapochemka huendelea tu kupambana ili kuwapumbaza wanachama na wapenzi wao wasiwawashie moto- labda na hiki ndicho wanachotaka kufanya na Yanga SC kwa sasa.
Lakini kabla ya kufikiria kupoteza muda, nguvu na gharama zaidi katika suala ambalo wanajua kabisa waliteleza wao wenyewe, wafikirie na majukumu mazito yaliyo mbele yao.
Mwishoni mwa wiki wana mechi ya Ngao ya Jamii na Azam FC. Wamecheza mechi za kirafiki nne, timu imeshinda zote lakini haijaonyesha kwango cha kufurahisha sana.
Wachezaji wapya waliosajiliwa ni mmoja tu, Coutinho ambaye amewafurahisha wapenzi, lakini wengine kama Jaja bado hawajaeleweka.
Yanga SC iliifunga KMKM 2-0 bao la pili dakika ya mwisho- lakini timu hiyo hiyo ikafungwa 5-0 na Simba na 4-0 na Azam FC.
Yanga iliifunga 1-0 kwa mbinde Thika United iliyomaliza nafasi ya saba katika Ligi ya Kenya msimu uliopita na siku iliyofuata Simba SC ikawafunga mabingwa wa nchi hiyo, Gor Mahia 3-0.
Inaonekana wazi Yanga SC wanakabiliwa na shinikizo la kuifanya timu yao iitwe tena bora Tanzania- kwa kuhakikisha inashinda vizuri na kucheza soka ya kuvutia.
Manji anasema ana uwezo wa kusajili wachezaji wote wa Simba SC, lakini hadi jana Yanga SC haijaingia kambini wakati inacheza mechi ya Ngao ya Jamii Jumapili Uwanja wa Taifa.
Simba SC imekuwa kambini Zanzibar kwa wiki mbili na iliporejea Dar es Salaam imeendelea kuwa kambini, wakati haijulikani ni kipi kiliifanya Yanga SC ikakatisha kambi yake Pemba baada ya wiki moja na kwenda Zanzibar kucheza mechi mbili za kirafiki kisha kurejea Dar es Salaam, ambako wachezaji hawakukaa kambini tena.
Wakati hayo yote bado yanawaumiza kichwa wana Yanga SC, Manji na uongozi wake bado wanataka kuendelea kupoteza muda kwa suala la Okwi. Hakuna haja, Yanga SC wasahau na wajipange kukabiliana na changamoto zilizo mbele yao. Tukijaaliwa Jumapili inshaallah.

0 comments:
Post a Comment