BONDIA Floyd Mayweather ametuhumiwa kumtesa, kutishia kumuua na kumuibia mpenzi wake wa zamani, Shantel Jackson kwa mujibu wa kesi iliyofunguliwa mahakamani.
Bondia huyo bingwa wa uzito wa madaraja matano tofauti ambaye hajawahi kupoteza pambano, anatarajiwa kupanda ulingoni wikiendi hii kuzipiga na Marcos Maidana akiwa anakabiliwa na hatari ya kutupwa jela baada ya mashitaka yaliyowasilishwa na mpenzi wake huyo wa zamani.
Anapambana na maisha yake: Floyd Mayweather ataanza kupanda kizimbani katika kesi yake dhidi ya mpenzi wake wa zamani, Shantel Jackson
Machozi: Jackson, mwenye umri wa miaka 29, akimwaga machozi wakati akitangaza kesi aliyomfungulia bondia huyo mjini Los Angeles
Mwanamitindo huyo mwenye umri wa miaka 29 alikuwa akizungumza huku akilia na kutaja jina Mayweather wiki iliyopita katika Mkutano na Waandishi wa Habari, akilalamika kupigwa na bondia huyo, na kubandika picha zake za faragha za vipimo vya ultrasound kwenye mitandao ya kijamii na kutangaza kwamba wameachana kwa sababu ametoa mimba ya watoto wao wawili pacha.
Lakini katika jalada lililofunguliwa mahakamani kilichosheheni katika uhusiano wa bondia huyo na mlimbwende huyo kwa miaka minane ni machungu tu.
Shantel anasema aliteseka mno mikononi mwa Mayweather, mwenye umri wa miaka 37, aliyekuwa akimpiga, hadi akamtegua bega, na wakati fulani alimtishia kumpiga bastola.
Pia alimuweka ‘jela’ nyumbani wake Las Vegas, na kutishia kuchapisha picha za uchi alizompiga mlimbwende huyo kwa siri wakiwa wamelala pamoja kitandani na kumuibia maelfu ya dola alizopokea kwa ajili yake.
0 comments:
Post a Comment