• HABARI MPYA

    Saturday, September 13, 2014

    PHIRI ASHINDWA KUVUNJA REKODI YA LOGARUSIC SIMBA SC

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    KOCHA Mzambia, Patrick Phiri jana amepoteza mechi ya kwanza ndani ya tano tangu aanze kuinoa klabu hiyo mwezi uliopita, akirithi mikoba ya Mcroatia, Zdravko Logarusic.
    Logarusic alifukuzwa mwezi uliopita baada ya kushiriki uundwaji wa kikosi cha msimu mpya- uongozi mpya wa Simba SC ukidai haendani na maadili ya klabu.
    Na kufukuzwa kwake kulikuja ndani ya saa 24 tangu Simba SC ifungwe 3-0 na ZESCO United ya Zambia katika tamasha la Simba Day.
    Kocha Patrick Phiri (kushoto) alirithi mikoba ya Zdravko Logarusic (kulia) aliyetupiwa virago mwezi uliopita Simba SC

    REKODI YA PATRICK PHIRI TANGU AREJEE SIMBA SC; 

    Simba SC 2-1 Kilimani City (Kirafiki Zanzibar)
    Simba SC 2-0 Mafunzo (Kirafiki Zanzibar)
    Simba SC 5-0 KMKM (Kirarfiki, Zanziabr)
    Simba SC 3-0 Gor Mahia (Kirafiki, Dar es Salaam)
    Simba SC 0-1 URA (Kirafiki, Dar es Salaam)
    Lakini Mcroatia huyo baada ya kujiunga na Simba SC Desemba mwaka jana akirithi mikoba ya Mzalendo, Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibadeni’ aliiongoza timu kushinda mechi tano mfululizo 3-1 na KMKM, 3-1 na Yanga SC, 1-0 KMKM, 2-0 Chuoni na 2-0 URA kabla ya kufungwa mechi ya sita na KCC 1-0.
    Lakini Phiri baada ya kushinda 2-1 na Kilimani City, 2-0 na Mafunzo, 5-0 na KMKM na 3-0 na Gor Mahia, jana alikwama mbele ya URA kwa kichapo cha 1-0 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Kwa ujumla, hadi anaondoka, Logarusic aliiongoza Simba SC katika mechi 21, kati ya hizo akishinda nane, kufungwa nane na sare tatu.  
    Lakini Logarusic hakuipa Simba SC taji lolote, katika miezi yake saba ya kuwa kazini, wakati Phiri sasa ndiyo anaanza kampeni ya kuwapa Wekundu wa Msimbazi taji la kwanza baada ya misimu miwili ya ukame.
    Kipa Ivo Mapunda akiwalaumu mabeki wake baada ya kufungwa jana Uwanja wa Taifa

    Kitu kimoja tu ambacho labda itawachukua muda mashabiki wa Simba SC kumsahau Logarusic, ni kwamba hakufungwa na Yanga SC, mechi moja akishinda 3-1 na moja akitoa sare ya 1-1 tena watani wao, wakichomoa dakika za lala salama kwa bao la Simon Msuva baada ya Haroun Chanongo kutangulia kufunga.

    REKODI YA ZDRAVKO LOGARUSIC SIMBA SC

    Simba SC 3-1 KMKM (Kirafiki)
    Simba SC 3-1 Yanga SC (Mtani Jembe) 
    Simba SC 1-0 KMKM (Kombe la Mapinduzi)
    Simba SC 2-0 Chuoni (Robo Fainali Kombe la Mapinduzi)
    Simba SC 2-0 URA (Nusu Fainali Kombe la Mapinduzi)
    Simba SC 0-1 KCC (Fainali Kombe la Mapinduzi)
    Simba SC 0-1 Mtibwa Sugar (Kirafiki)
    Simba SC 1-0 Rhino Rangers (Ligi Kuu Bara)
    Simba SC 4-0 JKT Oljoro (Ligi Kuu Bara)
    Simba SC 1-1 Mtibwa Sugar (Ligi Kuu Bara)
    Simba SC 0-1 Mgambo JKT (Ligi Kuu Bara)
    Simba SC 1-1 Mbeya City (Ligi Kuu Bara)
    Simba SC 2-3 JKT Ruvu (Ligi Kuu Bara)
    Simba 3-2 Ruvu Shooting (Ligi Kuu Bara)
    Simba SC 0-0 Prisons (Ligi Kuu Bara)
    Simba SC 0-1 Coastal Union (Ligi Kuu)
    Simba SC 1-2 Azam FC (Ligi Kuu)
    Simba SC 1-1 Kagera Sugar (Ligi Kuu)
    Simba SC 0-1 Ashanti United (Ligi Kuu)
    Simba SC 1-1 Yanga SC (Ligi Kuu)
    Simba 0-3 ZESCO United (Kirafiki Simba Day)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PHIRI ASHINDWA KUVUNJA REKODI YA LOGARUSIC SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top