• HABARI MPYA

    Wednesday, September 17, 2014

    MKONGO ALIYEICHEZEA RWANDA AFUNGIWA MIAKA MIWILI HAKUNA KUGUSA MPIRA

    BAADA ya Rwanda kuondolewa katika hatua ya makundi kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani nchini Morocco, Agosti 17, mwaka huu, Kamati ya Maandalizi ya michuano hiyo imemfungia pia na mchezaji Etekiama Agiti Tady kwa miaka miwili.
    Mchezaji huyo alikutwa hatua ya kutumia majina mawili tofauti na kuwa na hati mbili za kusafiri za Rwanda na Kongo na licha ya Amavubi kufuzu hatua ya makundi ya mtoano, imeondolewa kwa kosa hilo.
    Magumashi zimemponza; Etekiama Agiti Tady au Dady Simeon Birori amefungiwa miaka miwili na CAF  

    Katika kikao chake cha leo mjini Addis Ababa, Ethiopia Kamati hiyo imeamua kumsimamisha Etekiama Agiti Tady kwa miaka miwili. 
    Mchezaji huyo amekuwa akiichezea AS Vita ya kwao Kinshasa kwa pasipoti ya Kongo, wakati huo huo anaichezea timu ya taifa ya Rwanda kwa jina lingine, Dady Simeon Birori akiwa na tarehe tofauti ya kuzaliwa pia.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MKONGO ALIYEICHEZEA RWANDA AFUNGIWA MIAKA MIWILI HAKUNA KUGUSA MPIRA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top